Dar es Salaam, Tanzania – Agosti 07, 2024 – Britam Insurance Tanzania na Bank of Africa zashirikiana kuongeza upatikanaji wa huduma za Bima za Afya Tanzania ziitwazo ‘Amani Health’ na ‘Afya Care’

Ushirikiano huo unalenga kuongeza wigo mpana kwa wateja wa ‘Bank of Africa’ ili kuhakikisha kuwa watu binafsi, familia, wafanyabiashara na vikundi rasmi wanapata huduma za afya zenye unafuu na viwango. ‘Afya Care’ na ‘Amani Health’ zitakidhi mahitaji mbalimbali ya matibabu ya wateja wa Bank of Africa, katika kupunguza gharama za kifedha wakati wa dharura zinazohusiana na afya.

Mkurugenzi Mtendaji wa Britam Insurance Tanzania, Farai Dogo alieleza kufurahishwa kwake na ushirikiano huo na kusema, "Tunafuraha kuungana na Bank of Africa nchini Tanzania ambapo tumeweza kuwaletea wateja wao huduma hizi muhimu za 'Afya Care' na 'Amani Health'. Ushirikiano huu unaendana na dhamira yetu ya kuhakikisha tunatoa huduma bora za afya kwa watanzania wote. Hivyo ushirikiano huu utatuwezesha kuwafikia watu wengi zaidi na kuwapa ulinzi wanaohitaji ili waishi maisha bora zaidi.”

Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Bi. Esther Cecil Maruma, alisema “Ushirikiano wetu na Britam Insurance Tanzania ni uthibitisho wa ari yetu ya kutoa huduma za kipekee kwa wateja wetu, kupitia ‘Afya Care’ na 'Amani Health'. Hii sio tu kwamba tunaboresha utoaji wa bidhaa zetu lakini pia tunahakikisha kwamba wateja wetu wanapata huduma muhimu za afya. Mkakati huu unaonesha dhamira yetu ya kuboresha ustawi kwa wateja wetu na jamii inayotuzunguka."

“Bidhaa hizi zitapatikana kwa wateja wetu kuashiria hatua kubwa ya kuongeza upatikanaji wa huduma za afya na kuongeza wigo wa bima nchini Tanzania” akisistiza Bi. Eva Daudi Kakwale, Afisa Mkuu wa Idara ya Bima wa Bank of Africa Tanzania.

George Mwita, Meneja wa Idara ya Afya, Britam Insurance Tanzania, alisema “Tunaamini kwamba ushirikiano huu utaongeza kiwango kipya cha bima ya afya nchini Tanzania. Uzinduzi wa bima hizi ni sehemu ya mkakati unaoendelea katika kuboresha upatikanaji wa huduma ya afya na huduma ya bima nchini Tanzania huku tukiunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha bima ya afya inapatikana kwa watu wote. Britam Insurance Tanzania na Bank of Africa Tanzania zimejitolea kuhakikisha kuwa bidhaa hizi zinaleta matokeo chanya katika maisha ya wateja wao.

Kwa habari zaidi tafadhali tembelea matawi ya Bank of Africa na Britam Insurance Tanzania lililo karibu nawe.

Kuhusu Britam Insurance Tanzania:

Britam Insurance Tanzania ni kampuni inayoongoza kwa utoaji wa huduma za bima iliyo mstari wa mbele kutoa masuluhisho ya kibunifu na ya kina ya bima kwa watu binafsi na wafanyabiashara kwa kuzingatia ubora na kuridhika kwa wateja. Kampuni ilianzishwa mwaka 1998, Britam Insurance Tanzania inatoa bidhaa mbalimbali, ikiwa ni pamoja na afya na bima ya jumla katika mikoa 6 nchini Tanzania ikijumuisha Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Arusha, Mtwara na Mbeya.

Kuhusu Bank of Africa Tanzania

Ni taasisi ya kifedha inayotoa huduma mbalimbali za kibenki kwa wateja wake. Inapatikana kupitia matawi mbalimbali yaliyosambaa kote Tanzania, Bank of Africa inatoa huduma na usaidizi wa kipekee kwa watu binafsi, wafanyabiashara na jamii.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...