Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, amekutana na kufanya mazungumzo na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Bankers Without Boundaries (BWB) kutoka Uingereza, Bw. Chris Smith, ambapo wamejadili masuala ya ushirikiano wa kimaendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo Afya, elimu, Uchumi na maendeleo ya kijamii.
Mazungumzo hayo ambayo yamefanyika jijini Dodoma yamehudhuriwa na Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Madeni, Bw. Japhet Justin, Mkurugenzi wa Taasisi ya BWB, Bw. Matteo Scalabrino na wajumbe wengine kutoka pande hizo mbiliKatibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kulia) akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Bankers Without Boundaries (BWB) kutoka Uingereza, Bw. Chris Smith (katikati), baada ya kumalizika kwa mkutano kati yao ambapo wamejadili masuala ya ushirikiano wa kimaendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu, uchumi na maendeleo ya kijamii, jijijini Dodoma. Kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya BWB, Bw. Matteo Scalabrino.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (kushoto) akiongoza kikao kati yake na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Bankers Without Boundaries (BWB) kutoka Uingereza, Bw. Chris Smith (kulia), ambapo wamejadili masuala ya ushirikiano wa kimaendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu, uchumi na maendeleo ya kijamii, jijijini Dodoma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Bankers Without Boundaries (BWB) kutoka Uingereza, Bw. Chris Smith, akieleza kuhusu mikakati ya taasisi hiyo katika kuchochea maendeleo ya jamii, wakati wa mkutano kati yake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (hayupo pichani), jijini Dodoma.
Wajumbe kutoka Wizara ya Fedha wakiwa katika mkutano kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Bankers Without Boundaries (BWB) kutoka Uingereza, Bw. Chris Smith (hawapo pichani), ambapo wamejadili masuala ya ushirikiano kimaendeleo, jijijini Dodoma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Bankers Without Boundaries (BWB) kutoka Uingereza, Bw. Chris Smith (kulia), akiwa ameambatana na wajumbe wengine wakati wa mkutano kati yake na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba, ambapo wamejadili masuala ya ushirikiano wa kimaendeleo, jijijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba (wa tano kulia) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Bankers Without Boundaries (BWB) kutoka Uingereza, Bw. Chris Smith (wa tano kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka Wizara ya Fedha na Taasisi ya BWB, baada ya mkutano wao jijini Dodoma, ulioangazia ushirikiano wa kimaendeleo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...