Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Kamishna Benedict Michael Wakulyamba, amepongeza juhudi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika kuimarisha usimamizi wa hifadhi za mikoko na utalii wilayani Tanga.

Katika ziara yake hiyo, Kamishna Wakulyamba alitembelea ofisi ya TFS Wilaya ya Tanga na kukutana na Mhifadhi wa Wilaya pamoja na watumishi wa wakala, na kupokea taarifa za utendaji kwa mwaka wa fedha 2024/2025 na kujionea maendeleo ya miradi ya uhifadhi na utalii.

Mhifadhi wa TFS Wilaya ya Tanga, Lawlence Brighton Kamugisha alieleza kuwa wakala umeanzisha Kamati za Maliasili za Vijiji (VNRC) ili kuimarisha usimamizi wa hifadhi za mikoko kwa kushirikiana na wananchi. 

Aliongeza kuwa TFS imeanzisha miradi rafiki kwa mazingira, ikiwemo uanzishwaji wa mizinga ya nyuki, kama njia ya kupunguza utegemezi wa kifedha kwa jamii.

"Wakala umeimarisha doria za majini kwa kununua injini mpya yenye nguvu ya HP 115 na kufanya matengenezo makubwa ya boat ya doria, ili kuboresha ulinzi katika wilaya za Mkinga, Tanga, na Pangani," alisema Mhifadhi huyo.

Baada ya kupokea taarifa na kujionea shughuli za uhifadhi, Wakulyamba alikemea uvamizi wa eneo la hifadhi la Chumvini, ambapo wananchi wameanzisha makazi na kuharibu mazingira, huku akitia wito kwa wahifadhi kufuata taratibu, sheria, na kanuni za uhifadhi kwa weledi na kuzingatia mila na desturi za kiaskali.

"Wahifadhi mnapaswa kufanya kazi kwa weledi, kufuata taratibu, sheria, na kanuni za jeshi la uhifadhi. Ni muhimu kujua sheria mbalimbali za uhifadhi, ikiwa ni pamoja na sheria za wanyapori, General Orders, na sheria za ushahidi," alisisitiza Wakulyamba.

katika hatua nyingine Wakulyamba alikubaliana na mipango ya kuanzisha zao jipya la utalii katika hifadhi ya mikoko, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa boardwalk yenye mita 150 na maboresho ya kituo cha Malikale Tongoni. 

Aidha. alishukuru kwa uimarishaji wa doria za majini na kuwataka watumishi kuongeza majengo katika Mangrove Boardwalk ili kuvutia wageni zaidi na kuongeza mapato.

Naibu Katibu mkuu pia Katika ziara yake alitembelea ofis za wilaya  za TFS Pangani ambapo alipongeza jitihada za jitihada za kiuhifadhi zinazofanywa na TFS Katika uhifadhi na usimamizi wa uvunaji na kuvuka lengo la MAKUSANYO ya Fedha za serikali, pia alisisitiza uimarishaji wa doria kudhibiti utoroshaji wa mazao ya misitu Kwa njia ya bandari zisizo rasmi.

Katika ziara hiyo Naibu Katibu mkuu aliambatana na Maafisa waandamizi toka makao makuu TFS na Kanda.








Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...