Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amezungumzia umuhimu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kushirikiana na wananchi kulinda hifadhi za barabara na hivyo kuwezesha ujenzi wa miundombinu hiyo kufanyika kwa urahisi na kudumu kwa muda mrefu.

Akikagua ujenzi wa barabara ya Mkuranga-Kisiju KM 45 na barabara ya Kilwa mkoani Pwani amehimiza ushirikishwaji wa wananchi katika kulinda hifadhi ya barabara ili kuepuka uvamizi wa hifadhi hizo hali inayosababisha uchimbaji wa mchanga na mawe na hivyo kuathiri barabara na madaraja wakati wa mvua.

" TANROADS waelimisheni wananchi ili wazuie wenzao kulima, kujenga na kuchunga mifugo kwenye hifadhi za barabara ili kulinda barabara na kuzikarabati kwa urahisi inapohitajika", ameelekeza Kasekenya.

Mkoa wa Pwani ni mkoa wa Viwanda hivyo ujenzi na ukarabati wa barabara hizi za Kilwa na Mkuranga-Kisiju KM 45 uzingatie ubora na viwango vya juu ili kuwezesha magari makubwa kusafirisha malighafi na bidhaa za viwandani kwa urahisi wakati wote.

" Kukamilika kwa barabara ya Mkuranga -Kisiju kutaongeza tija kwenye bandari ya kisiju na hivyo kuvutia wawekezaji wa Viwanda na Hotel", amesisitiza Naibu Waziri Kasekenya.

Naibu Waziri Kasekenya amesema Serikali iko katika hatua za mwisho kwa kushirikiana na Benki ya Dunia kufanya ukarabati mkubwa kwenye maeneo yote ya barabara na madaraja yalioathiriwa pakubwa na mvua zilizonyesha mwaka huu.

Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani Eng. Zilli Kihoko amesema watahakikisha hifadhi za barabara, maeneo ya maegesho na madaraja yanalindwa ili yadumu na kuleta tija kwa wananchi.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...