Na WAF - Dar Es Salaam
Zoezi la utoaji wa huduma za kibingwa kwenye Hospitali 184 ngazi ya Halmashauri kupitia mpango kabambe wa "Madaktari bingwa wa Dkt. Samia limepunguza mateso na kukomboa wagonjwa wengi, hasa wale walioteseka kwa ugonjwa wa uvimbe wa muda mrefu.
Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amesema hayo leo Agosti 7, 2024 wakati akitoa taarifa juu ya madaktari bingwa wa Rais Samia kwa waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya Jijini Dar Es Salaam.
"Tumeshuhudia mawe yakiondolewa kwenye vibofu vya mikojo ikiwemo jiwe la ukubwa wa kilo 1 na gram 200, upasuaji wa Goita, watoto 20 wamefanyia upasuaji wa kurekebisha maumbile ya uume (hypospodiasis repair) ambayo yangeweza kusababisha ulemavu wa kudumu." Amesema Waziri Ummy
Aidha, Waziri Ummy amesema katika zoezi hilo takribani wagonjwa elfu 70 wamefikiwa ambapo kati yao, madaktari bingwa wa magonjwa ya ndani waliona wagonjwa 22,057 sawa na aslimia 32%, magonjwa ya wanawake na uzazi 18,044 (26%), watoto 14,466 (21%), na madaktari bingwa wa upasuaji waliona wagonjwa 10,578 (15%), Kwa ujumla wateja 4,652 (7%) walipata huduma za upasuaji.
Amesema, Mikoa 10 iliyoongoza kwa wagonjwa wengi waliojitokeza kuonwa na madaktari bingwa wa Rais Samia ni mkoa wa Tanga wateja elfu 4,410, Mara wagonjwa 3,671, Tabora 3,652, Mtwara 3,540, Mwanza 3,256, Ruvuma 3,253, Mbeya 3,126, Kagera 3,122, Pwani 2,966 pamoja na Manyara wagonjwa 2,964.
"Zaidi ya hayo tumebaini, kati ya watoto 14,466 walioonwa, matatizo ya mfumo wa hewa na moyo yaliongoza kwa kuwa na wagonjwa 2,352 sawa na 16%, uambukizo wagonjwa 2,091 (15%), upungufu wa damu au Sickle Cell wagonjwa 1,287 (9%) na Nimonia wagonjwa 1,030 (7%)." Amesema Waziri Ummy.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...