Mshauri wa Rais Masuala ya Wanawake, Bi.Sophia Mjema akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa Manyala, Bi. Queen Sendiga wakati wa uzinduzi wa program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia {IMASA} inaendeshwa na Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), wapili kusho ni Katibu Mtendaji wa Barza hilo Bi. Beng’i Issa, . Picha na Mwndishi Wetu.
Na Mwandishi wetu, Manyala
MAKUNDI ya Kinamama, vijana na makundi maalum Mkoani Manyala yameaswa kuitumia Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) kwa kujisajili na kuingia katika kanzidata ili kupata uwezeshaji na badaye kunufaika na fursa zinazotolewa na halmashauri zao kwa nia ya kuondokana na hali duni ya vipato
Hayo yalisemwa na Mshauri wa Rais Masuala ya Wanawake, Bi.Sophia Mjema wakati wa uzinduzi wa program hiyo ya IMASA katika Mkoa wa Manyala ambayo inaendeshwa na Baraza la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC) kuwa makundia hayo yanahitajika kujisajili ili kupata uwezeshaji utakao wawezesha kutumia fursa za kibiashara na ujasirimali.
“Ninawaomba kinamama fungueni vikundi vyenu kisha msajili ili muweze kunufaika na fursa zinazotolewa na halmashauri zenu,” na aliongeza kusema mkoa huo unafursa nyingi jambo la msingi ni kukidhi vigezo vya kuzitumia fursa hizo kukuza biashara na ujasirimali, alisema.
Pia alizitaka Halmashauri kuhakikisha zinatoa kazi kwa makundi hayo ili yaweze kukuza biashara na ujasiliamali. “Wapeni kazi za kulisha makongamano, mikutano, kazi za ukandarasi ndogondogo kukarabati barabara mana watafungua vikundi vya ukandarasi, alisisitiza Mjema.
Alisema Serikali ya mama Samia kupitia baraza hilo inalenga kuyakwamua makundi hayo, jambo kubwa ni kuyasaidia makundi haya kupitia vikundi vyao kuingia katika mfumo rasmi na kisha kuwapatia kazi zinazopatikana katika halmashauri zao.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC),Bi. Beng’I Issa lisema baraza limejipanga kupitia program hiyo kuhakikisha mafunzo yanawafikiwa makundi hayo ili waweze kuendeleza shughuli za biashara na ujasirimali.
“Mkoa wa Manyala unafursa nyingi za kiuchumi zikitumiwa vizuri hasa baada ya kupata mafunzo ya biashara na ujasirimali watafanya vizuri zaidi, na kwa kupitia program hii kwa kushirikiana na halmashauri zao wataweza kufikia ndoto zao kiuchumi.
Mkuu wa Mkoa Manyala, Bi. Queen Sendiga alipongeza baraza kwa kuzindua program hiyo katika mkoa wake na atahakikisha anashirikiana na makundi hayo kuhakikisha uwezeshaji unaofanywa na IMASA unafanikiwa katika mkoa wake.
“Katika mkoa wetu tumeipokea program ya IMASA kwa mikono miwili na tutafanyakazi kuhakikisha malengo yake yanatimia,” IMASA ni mkombozi wa makundi haya kikubwa makundi haya na watumishi wa serikali ni kufanya kazi kwa karibu, alioneza kusema.
Mfugaji kutoka Babati, Bw, Naye Colman Maso alisema anaufuga ng’ombe kisasa na hata majilani zake nao wafanya shughuli za kilimo na ufugaji na anafurahi kupata mafunzo hayo kutoka program hiyo kuwa yamemwongezea tija ya kazi.
Naye Bi.Clara Mali kutoka kata ya Mamile Wilaya ya Babati anasema yeye ni mkulima na pia anafanya kazi za salon anapamba maharusi na kuwasuka, kuweka dawa nywele na kuweka maua vizuri, alisema amejifunza umuhimu wa kuwa na akauti benki na pia amejifunza juu ya fursa mbalimbali zilizopo.
“Program hii inalenga pia kutuwezesha mafunzo na mitaji,” na aliongeza kwa kusema vijana na akinamama wapo tayari kuitumia fursa hii ili kupata mafunzo na mitaji kukuza biashara na ujasiriamali.
Vilevile Mama Lishe kutoka Wilaya ya Babati, Bi. Afsa Mbisha anasema analihukuru baraza kwa kuwaletea program ya IMASA ambayo iliwapa mafunzo ya ujasirimali ikiwemo kujiamini, kutunza fedha katika kaunti benk, kusajili vikundi na kupata uwezeshaji.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi {NEEC}, Bi. Beng’i Issa kizungumza na makundi ya kimamama, vijna na mkundi maalum hayapo pichani Mkoani Manyala wakati baraza hilo lilipozindua Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia {IMASA} inayotekelezwa na Baraza hilo. Picha na Mwandishi Wetu Mnyala.
Makundia ya kimamama, vijna na mkundi maalum ya Mkoani Manyala wakishiriki mafunzo ya ujasiriamali wakati Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi {NEEC} lilipozindua Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia {IMASA} mkoani humo. Picha na Mwandishi Wetu Manyala.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...