Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya amhakikishia Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi kuwa Serikali imepanga kufungua mkoa wa Geita kwa barabara za lami ili kurahisisha huduma za usafiri na uchukuzi hivyo kukuza uchumi wa Mkoa huo.

Akizungumza na wananchi wa mji wa Katoro mkoani humo Eng. Kasekenya amesema nia ya Serikali nikuhakikisha maeneo yote yenye uzalishaji na biashara kubwa yanafikika kirahisi kwa Barabara za lami ili kuleta tija na ufanisi kwa wananchi.

" Mhe. Katibu mkuu mwaka huu tumejipanga kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami barabara za Nzera-Nkome Km 20, Mtakuja-Bukoli- Bulyanhulu-Busoka-Kahama KM 122.7 na Ushirombo-Katoro 58.3", amesema Naibu Waziri Kasekenya.

Naibu Waziri huyo amewataka wakazi wa Mkoa wa Geita kutumia fursa ya ujenzi wa barabara hizo kupata ajira na kukuza shughuli za biashara, uzalishaji na huduma ili kukuza uchumi binafsi na wa mkoa wa Geita kwa ujumla.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...