KATIBU wa Bunge, Nenelwa Mwihambi amesema bunge lina mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta ya kilimo nchini.
Hayo aliyasema leo jijini hapa wakati alipotembelea maonyesho ya nanenane katika viwanja vya nzuguni ambapo alisema bajeti inayotumika kwenye shughuli hizo kwa kiasi kikubwa inatokana na bunge.
Alisema jukumu kubwa la bunge ni kuishauri serikali na kuisimamia na kwamba kupitia kamati wabunge wamekuwa wakitoa ushauri wa namna ya kuboresha shughuli za kilimo kwa ajili ya manufaa ya nchi na ajenda za kimkakati.
“Maswali yamekuwa yakiulizwa bungeni na wabunge serikali imekuwa ikitoa fafanuzi mbalimbali kwa wabunge wanaotoka maeneo ya kilimo.”
Alibainisha kuwa maonyesho ya mwaka huu yamefana kutokana na mabadiliko makubwa yaliyofanyika tofauti na siku za nyuma kulikuwa na vumbi na barabara hazikuwa vizuri.
“Naipongeza wizara ya kilimo na ofisi ya mkuu wa mkoa wa uratibu mzuri ambao wameufanya, sisi kama bunge tumepata wageni sana hususani wanafunzi wamekuja kujifunza, nazidi kuwahamasisha wananchi wafike banda la bunge kupata taarifa mbalimbali.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...