Naibu Waziri Wa Uchukuzi David Kihenzile amesema Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na Sekta Binafsi kwa kuweka mazingira wezeshi ili kuhakikisha Sekta ya anga inakua na kuendelea kuchangia katika pato la Uchumi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mara baada ya kutembelea anga ya kampuni ya Ndege ya Precision, kukutana na kuzungumza na Wakurugenzi watendaji wa Coastal Aviation na Flightlink Naibu Waziri Kihenzile amesema Uwekezaji unaofanywa na Serikali kwenye eneo la kuboresha Miundombinu ya Viwanja utakuwa na matokeo makubwa pale ambapo Sekta Binafsi pia itawekeza katika ununuzi wa ndege.

Naibu Waziri Kihenzile ameongeza kuwa Serikali iko katika hatua mbalimbali ya kufanya maboresho kwenye sera ya Uchukuzi ma sheria ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege kwa Lengo la kuimarisha Sekta ya usafiri wa anga.

Naye Mkurugenzi wa Precision Patrick Mwanri amesema katika mpango kazi wake imepanga kuongeza Ndege ambazo zitakwenda sambamba na ongezeko la vituo ambavyo kampuni itakuwa ikitoka Huduma Nchini.

Mkurugenzi Mwanri ameiomba Serikali kupitia Naibu Waziri Kihenzile kuzisaidia kampuni Binafsi za ndege kuweza kupata mikopo kupitia benki za ndani ili kuziimarisha kwenye Uendeshaji.

Kwa upande Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Flight link Kaptenj Munawer Dhirani ameishukuru Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutekeleza dhamira yake ya kuweka mazingira mazuri ya Sekta ya anga na kuhakikisha makampuni Binafsi yanaendelea kuwekeza kwa kununua Ndege Nchini.

Kapteni Munawer ameongoza kuwa  mazingira yaliyowekwa yameiwezesha Kampuni ya Flightlink kuweka mipango ya  kuongeza mtandao wa safari ambapo mapema mwisho wa mwaka Kampuni hiyo itaongeza kituo cha Mwanza.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe.David Kihenzile  akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Precision Air, Bw. Patrick Mwanri alipotembelea karakana ya matengenezo ya ndege ya Precision Air iliyopo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijii Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe.David Kihenzile  akisaini kitabu cha wageni  alipotembelea karakana ya matengenezo ya ndege ya Precision Air iliyopo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijii Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe.David Kihenzile akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege la Precision Air, Bw. Patrick Mwanri alipotembelea karakana ya matengenezo ya ndege ya Precision Air iliyopo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijii Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe.David Kihenzile akipata maelezo mbalimbali kuhusu karakana ya  Shirika la Ndege la Precision Air alipotembelea karakana ya matengenezo ya ndege ya Precision Air iliyopo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijii Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe.David Kihenzile akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Precision Air alipotembelea karakana ya matengenezo ya ndege ya Precision Air iliyopo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijii Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe.David Kihenzile akizungumza na uongozi wa Kampuni ya Flight Link ukiongizwa na  Mkurugenzi Mtendaji Munawer Dhirani Flight link alipotembelea ili kuona huduma mbalimbali wanazozitoa pamoja na kusikiliza changamoto wanazozipitia wawekezaji kwenye Usafiri wa Anga hapa nchini.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe.David Kihenzile akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Flight Link Munawer Dhirani  alipotembelea kampuni  hiyo ya ndege ili kuona huduma mbalimbali wanazozitoa pamoja na kusikiliza changamoto wanazozipitia wawekezaji kwenye Usafiri wa Anga hapa nchini.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe.David Kihenzile akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Munawer Dhirani Flight link alipotembelea ili kuona huduma mbalimbali wanazozitoa pamoja na kusikiliza changamoto wanazozipitia wawekezaji kwenye Usafiri wa Anga hapa nchini.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe.David Kihenzile akiwa kwenye picha ya pamoja na uongozi wa Kampuni ya Flight Link ukiongozwa na  Mkurugenzi Mtendaji Munawer Dhirani Flight link alipotembelea ili kuona huduma mbalimbali wanazozitoa pamoja na kusikiliza changamoto wanazozipitia wawekezaji kwenye Usafiri wa Anga hapa nchini.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe.David Kihenzile akipokelewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Coastal Aviation Dkt. Capt. Basil Obeidat alipotembelea kampuni hiyo ya ndege ili kuona huduma mbalimbali wanazozitoa pamoja na kusikiliza changamoto wanazozipitia wawekezaji kwenye Usafiri wa Anga hapa nchini.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe.David Kihenzile akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Coastal Aviation Dkt. Capt. Basil Obeidat alipotembelea ili kuona huduma mbalimbali wanazozitoa pamoja na kusikiliza changamoto wanazozipitia wawekezaji kwenye Usafiri wa Anga hapa nchini.
Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe.David Kihenzile akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Coastal Aviation Dkt. Capt. Basil Obeidat alipotembelea kampuni  hiyo ya ndege ili kuona huduma mbalimbali wanazozitoa pamoja na kusikiliza changamoto wanazozipitia wawekezaji kwenye Usafiri wa Anga hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...