Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, walioteuliwa ni kama ifuatavyo:-
Prof. Faustin Rweshabura Kamuzora ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Uwekezaji ya UTT – AMIS. Prof. Kamuzora ni Katibu Tawala wa Mkoa Mstaafu, anachukua nafasi ya Bw. Casmir Kyuki ambaye amemaliza muda wake;
Prof. Joseph Andrew Kuzilwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP). Prof. Kuzilwa ni Profesa Mstaafu, Chuo Kikuu cha Mzumbe; na
Prof. Ahmed Mohamed Ame ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) kwa kipindi cha pili.
Uteuzi huu umeanza tarehe 04 Agosti, 2024.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...