Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi {NEEC} kupitia programa ya Imarisha Uchumi na Mama {SAMIA)imeyataka makundia ya kinamama, vijana na makundi maalum Mkoani Kilimanjaro kuongeza ubunifu katika shughuli za biashara na ujasirimali ili kuweza biashara kubwa na kuwa maisha mazuri katika familia zao.
Hayo yalisemwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Bi. Beng’i Issa wakati wa uzinduzi wa Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia {IMASA} mkoani humo ambayo inatekelezwa na baraza hilo kuwa ubunifu katika kukuza biashara zao.
“Tunatambua Mkoa wa Kilimanjaro unafursa za kibiashara hasa katika utalii, kilimo cha kahawa na mazao mengine,” na aliongeza kusema, Bi. Beng’i kuwa katika kufanya shughuli hizi wanahitajika kuboresha shughuli hizo ili kukidhi mahitaji ya wateja.
Alisema katika mkoa huo sekta ya utalii imeshamili ambapo watalii wanapanda mlima Kilimanjaro ambao hutoa fursa kubwa kwa wasafirishaji wa watalii, wataoa huduma ya chakula, maradhi na burudani ambapo serikali hupata fedha za kigeni.
Bi. Beng’i alifafanua kwamba wafanyabiaashara wadogo wa mkoa huo wanapongezwa kwa kujenga uaminifu katika kuwahudumia watalii ambao hata hawakutani na matendo ya kuibiwa mizigo badala yake wafanyabiashara hao wanasifi kwa tabia njema.
Pia alisema fursa ya mazao kama kahawa yenye masoko nje ya nchi yanaangaziwa na program hiyo ili yaweze kupata uwezeshaji na kuwapa mafanikio kwa watu wanaojishughulisha nayo waweze kuwa matajiri.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro, Bw. Nurdin Babu alisema mkoa wake umeipokea program kwa mikono miwili na watafanya kazi ili waweze kuwa wakwanza kuingia katika program kwa nia ya wananchi wao kunufaika na fursa hiyo.
“Program hii imeletwa katika mkoa wetu hivyo napenda kuwaambia wananchi tutashirikiana kuhakikisha mnanufaika na program,” na nawataka wakuu wa wilaya, wakurugenzi, na viongozi wa usafirishaji bajaj tuzidi kuboresha huduma katika sekta ya utalii.
Mshauri wa Rais Masuala ya wanawake Sophia Mjema aliyataka makundi hayo yawe yamejiunga vizuri na kujisajili ili IMASA iweze kuwawezesha kulingana na shughuli za biashara na ujasirimali wanazofanya.
“Lengo la kuwataka kuwa katika makundi haya ni kutaka kuyawezesha katika shughuli mbalimbali zikiwemo za utalii na kilimo,” pia alisema mazao kama ya kahawa yanahitajika kuongezwa thamani ili kukidhi masoko nje ya nchi.
Alisema program hiyo imekuja kusaidia makundi hayo ambapo anayefanya usafirishaji kwa njia ya bodaboda ili badaye waweze kulimiki gari, mamalishe pia awe na mgahawa.
Bi.Winie Masawe Mkazi wa Moshi Mjini Mkoa wa Kilimanjaro alisema anaamini IMASA itamwinua katika shughuli zake za biashara za kutengeneza sabuni za maji na karanga za mayani.
“Mimi nimejiajiri na ninamwaka mmoja sasa matumaini yangu kupitia IMASA mtaji wangu utakua na kuweza kutimiza ndoto zangu kiuchumi,”alifafanua Bi.Masawe.
Bw. Shukuru Gau alisema yeye ni mjasirimali na amepta kujifunza mafunzo ya ujasiriamali na anahitaji kujikwamua kiuchumi kupitia biashra ndogondogo.
Wafanyabiashara wadowadogo wanashindwa kukua kutokana na tatizo la mtaji lakini kupitia program hiyo tutakua kibiashara na nawaomba vijana wenzake waingiekatika program hiyo.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...