Na mwandishi wetu, Arusha
Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kupitia Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) linalenga kuyaongeze uwezo wa biashara na ujasirimali makundi ya Kinamama, Vijana na makundi maalum wa Mkoani Arushi hasa wanaofanya shughuli za kitalii na biashara za nafaka zinazosafirishwa kwenda nchi za Afrika Mashariki.
Kauli hiyo ilitolewa na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Bi. Beng’i Issa wakati wa Baraza hilo lilipozindua Program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) inayotekelezwa na baraza hilo kuwa Mkoa wa Arusha kuwa makundi hayo yataongezewa uwezo w kibiashara hasa katika maeneo ya utalii na nafaka zinazounzwa nje ya nchi.
“Mkoa huu wa Arusha ni wa kimataifa na umeshamili shughuli za kitalii na mpaka wa kusafirisha mazao ya nafaka kwa nchini za Afrika Mashariki,” na alioneza kusema program hiyo inalenga kuwaongezea ujuzi na uwezeshaji ili waweze kutumia fursa kama hizo kwa mafanikio makubwa zaidi.
Alisema Royal Toure aliyofanya Rais Mama Samia ilikuwa na mafanikio makubwa katika mkoa huo ambao ni Jijiji kwa hiyo program zote zinazolisha utalii zitatapata mafanikio kupitia utalii na IMASA imejielekeza kwa wafanyabiashara wadogo wadogo na wajasirimali katika sekta hiyo wanufaike na kufikia viwango vya kimataifa.
Alifafanua kwamba Arusha ni jiji na makundi ya kinamama, vijana na makundi maalum yamekuwa na mwamuko na shughuli zao hasa akinamama kwa vile jiji linapokea watalii wanaposhuka, mikutano ya kitaifa na kimataifa inafanyika hapo.
Pia alisema akinamana wengi wanafanya shughuli za kuuza nafaka nje ya nchi na Tanzania ndiyo inayolima mazao ya nafaka na kulisha nchi za Afrika Mashiriki na Afrika ya Kati.
Amesema Tanzania na Kenya ni fursa nzuri katika maendeleo ya uchumi kwa watanzania kuvuka mpaka na kufanya biashara nchi nyingine.
Mshauri wa wa Rais Masuala ya Wanawake, Bi. Sophia Mjema alisema wale wote walioanjiandikisha wataingizwa katika kanzidata na kutaka makundi hayo kuchaangamkia fura hiyo kupitia IMASA.
“IMASA imejipanga kutoa uwezeshaji kwa akinamama, vijana na makundi maalum na hasa akinamama na hakuna atakaye achwanyuma,” na aliongeza kusema kila mmoja katika mtaa wake, kitongoji chake, Wilaya yake anahitajika kujiandikisha kuingia katika mfumo.
Naye Bi. Sophia Amiri Makazi wa Arusha alisema wamepokea mafunzo kutoka IMASA na wanaona kuwa inalenga kuwakwamua watanzania akinamama ambao bado wapo chini.
” Program inataka kutunyanyua akimama na makundi mengine na itamwezesha mwanamke anayeishi katika nyumba ya nyasi kuishi katika nyumba ya bati,” na aliongeza kusema anampongeza Rais Mama Samia kupitia baraza hilo kwa kupelekea program hiyo
Alisema katika mkoa huo akinamama wanajishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi na ujio wa program hiyo inawawezesha kupata maarifa na uwezeshaji kukuza biahara na ujasirimali.
Baraza la Uwezahaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kupitia program ya IMASA ipo katika hatua ya kutoa mafunzo kwa makundi ya kinamama, vijana na Makundi Maalumu na kuwaingiza katika kanzidata na badaye watapatiwa uwezeshaji ili waweze kukuza shughuli za biashara na ujasiriamali,
Alisema mkoa huo makundi hayo yalionyesha mwitikio mkubwa wa kuipokea program ya IMASA na inakadiliwa kulikuwa zaidi ya washiriki 1500 wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na wanaume.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC}, Bi.
Beng’i Issa akizungumza na mwakundi ya kinamama, vijana na makundi
maalum wakati baraza hilo lilipozindua Program ya Imarisha Uchumi na
Mama Samia mkoani Arusha. Picha na Mwandishi wetu, Arusha.
Makundi ya akinamama, vijana na Makundi maalum wakiwa katika uzinduzi wa program ya Imarisha Uchumi na Mama Samia (IMASA) katika Mkoa wa Arusha program hiyo inatekelezwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC). Picha na mwandishi wetu, arusha
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...