Na Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nelson Cosmas Mlali amesema kuwa watawakutanisha wadau mbalimbali wa usafirishaji kwa njia ya majini ili kuangalia namna bora ya kuweza kupunguza viwango vya Tozo ambavyo ndio moja kati ya vitu ambavyo vimekuwa vikilalamikiwa sana ili kuzifanya bandari zisiwe ghali katika kutumika na kumudu ushindani uliopo katika ukanda wetu.

Mlali ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akizungumza na Wanahabari mara baada ya maadhimisho ya kilele cha siku kuu ya Wakulima 88 iliyofanyika Kitaifa Jijini Dodoma katika viwanja vya Nanenane-Nzuguni.

Ameongeza kuwa wao kama TASAC wanawasimamia wadau mbalimbali wanaohusika katika mnyororo wa usafirishaji kwa njia ya maji,lakini zipo tozo mbalimbali kama tozo za bandari, bandari kavu na tozo za ukaguzi wa bidhaa ambazo zimekuwa zikipigiwa kelele na wadau hao.

"Sisi kama Shirika la Uwakala wa Meli walipozungumzia tozo kimsingi sio tu za TASAC lakini kwa wadau mbalimbali wanaohusika katika mnyororo wa usafirishaji kwa njia ya maji,kwasababu sisi tunasimamia wadau mbalimbali, mfano zipo tozo za bandari,bandari kavu na tozo za ukaguzi wa bidhaa ambayo ni mashirika mbalimbali sasa kwa kuwa zote hizo zinatumika katika usafiri wa maji basi utakuta kilio kile kinakuja kwa TASAC ".

"Kwahiyo tutakachofanya sisi ni kukutana na hao wadau wote na kujaribu kuangalia namna bora ya kuweza kupunguza tozo ili kuzifanya bandari zetu zisiwe ghali katika kutumika nchini na kwa kufanya hivyo tuweze kumudu ushindani uliopo katika ukanda wetu".

Aidha amebainisha baadhi ya changamoto walizopokea katika maonesho haya kuwa ni viwango vya tozo,ucheleweshaji wa meli kupata nafasi ya kupaki na uchelewaji wa magari katika mipaka na kusema kuwa watawakutanisha wadau hao wa usafirishaji wa majini na kujadili kuhusiana na viwango vya tozo mbalimbali zinazopatikana katika mnyororo mzima wa usafirisha wa mizigo yao kwa usafiri wa njia ya Bahari.

"Changamoto tulizopokea katika maonesho haya zipo za aina nyingi ikiwemo na kuhusiana na viwango vya tozo mbalimbali zinazopatikana katika mnyororo mzim wa usafirishaji wa mizigo yao kwa usafiri wa njia ya bahari. Lakini kingine ucheleweshaji labda wa meli kupata eneo la gati kwamba lazima zisubiri kule nje nafasi ya kuegesha ma nyingine ni utendaji mdogo ikiwemo kuchelewesha magari katima mipaka yanapotoka bandarini".

Pia Mkurugenzi huyo amesema moja ya malengo yao kuja katika maonesho haya ni kuja kutoa elimu kwa watumiaji usafiri wa njia ya maji na kujifunza changamoto mbalimbali wanazopitia wadau wanaotumia usafiri wa maji.

"Tumekuja kushiriki maonesho haya kwasababu ya kutaka kutoa elimu kwa wadau wanaotumia usafiri kwa njia ya maji kwamba wanapopata shida au maswali waifuate TASAC kwahili ya kupata ufafanuzi. Lakini pia tulitaka kujifunza changamoto mbalimbali wanazopitia wadau hao".

Sambamba na hayo ametumia fursa hii kutoa kwa Watanzania kwamba popote pale wanapoona TASAC ipo wajongee ili kuweza kupata elimu na suluhisho juu ya adha wanazokutana nazo pindi wanapotumia usafiri wa maji.

"Labda nitumie fursa hii adhimu kutoa wito kwa Watanzania kwamba wajitahidi wanapoiona TASAC wajongee ili waweze kuoata elimu na suluhisho juu ya changamoto wanazozipata pindi wanapotumia usafiri wa maji na tunaomba ushirikiano waoa hasa wale walioko karibu na maji iwe pwani za bahari au maziwani wawe mstari mbele katika kuhakikisha fukwe zetu zinakuwa salama na ili kudumisha usafiri lwa njia ya maji".

Dira ya TASAC ni kuwa Mdhibiti wa Usafiri wa Majini na viwango vya Ubora wa Kimataifa na kuwezesha Tanzania kuwa kitovu cha Usafiri Majini Duniani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...