Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la Bidhaa Tanzania - TMX Godfrey Marekano ameeleza kuwa maandalizi ya uuzaji na uunuzi wa Korosho msimu 2024/25 yameanza na yanaendelea vizuri.

Marekano amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam Agosti 13,2024 Jijini Dar es Salaam, huku akiwataka wakulima wa Korosho kuhakikisha kuwa wanazingatia ubora ili kuziongezea thamani Sokoni.

"Tumekuwa na simu mzuri katika mazao mengine kama Kahawa,Ufuta, Cocoa na sasa Mbaazi, lakini wakati huohuo tumeshaanza maandalizi kwa ajili ya uuzaji wa Korosho kwa mfumo wa kielektroniki, naweza kusema maandalizi yanaenda vizuri " amesema Marekano.

Kuhusu utaunzaji wa Korosho ghafi, amewashauri wakulima kuhakikisha kuwa wanazingatia ubora pale watakapoanza mavuno ili kuendelea kuwavutia wanunuzi.

"kama nilivyoeleza kwenye mazao mengine, hata kwenye Korosho ni hivyohivyo, Wakulima waache udanganyifu,wasichanganye Korosho na uchafu mwingine usiofaa, wanunuzi wanafuatilia na wanazingatia sana ubora ili fedha wanayotoa iendane sambamba na thamani ya kile walichonunua" amesisitiza Marekano


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...