SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wamezindua mafunzo ya uchumaji fedha kupitia mitandao ambapo baadhi wameshaanza kulipwa mwezi huu.

Akizungumza leo Agosti 15, 2024 Jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa  Tehama kutoka Wizara ya Habari Mwasiliano.na Teknolojia, Dkt. Nkundwe Mwasaga amesema amesema watumiaji wa meta wapo zaidi ya bilioni 3.3 mpaka sasa na kueleza  watanzania wana kila sababu ya kutumia mtandao huo kujiingizia kipato.

"Watu bilioni tatu ni sawa na idadi ya nchi fulani, hivyo kupitia Meta na   mafunzo haya tuna yatabadilisha watanzania mtazamo wao kuhusu uchumi wa kidigitali ambao ndio umeiteka dunia kwa  sasa ,"amesema Dkt. Mwasaga.

Kwa upande wake , Mwakilishi kutoka Unesco, Michel Toto, amesema shirika hilo litaendelea kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao.
 
"Unesco tunatambua mitandao ni fursa  kufanya shughuli zozote za uzalishaji mali, hivyo kuwapatia watu elimu hususani vijana kutawafanya wawe wabunifu katika kutengeneza maudhui yao," amesema Toto.

Nae Mkurugenzi wa Idara ya Ukuzaji wa maendeleo ya Sanaa Basata, Edward Muganga,  amesisitiza kutemgenezwa kwa maudhui yenye utanzania na kuzingatia maadili.

Pamoja na hayo kwa upande wake, Mwakilishi wa kampuni ya Meta inayoendesha mtandao huo, Desmond Mushi amesema watengeneza maudhui Tanzania katika mtandao wa kijamii Facebook  wameanza kulipwa mwezi huu wa Agosti,2024 na pia mtandao wa Instagram utaanza kuwalipa  mwezi ujao na hivyo watu kuwa na uwanja mpana wa kutengeza fedha kupitia mitandao ya kijamii.

Ameeleza kuwa atakayestahili kulipwa ni mtumiaji mwenye wafuasi kuanzia 5000 na kuendelea na kuanza kulipwa katika mtandao huo, kutaifanya Tanzania kuwa nchi ya tano Afrika ambayo watu wake wanalipwa.

"Tayari nchi ya Nigeria, Ghana , Kenya na Uganda zilishaanza kulipwa kabla yetu na sisi tumechelewa kwa sababu ya matumizi yetu ya lugha ya kiswahili lakini sasa tupo vizuri na tunaweza pia kutumia lugha hii kama fursa katika kuitangaza duniani,"amesema Mushi.

Amesema muhusika atalipwa kutokana na mambo manne ikiwemo anachoweka  kwenye ukurasa wake, matangazo ambayo yatawekwa kwenye maudhui yake na Meta.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...