NA WILLIUM PAUL, SAME.
WAZEE wilayani Same wametakiwa kukemea vijana wao kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa kujiepusha na vitendo vya kupokea au kutoa rushwa kushinikiza wagombea ili wawachague na badala yake washiriki kikamirifu kuchagua viongozi bora na waadilifu watakao simamia vyema fedha za miradi ya maendeleo zinazoletwa na Rais Dkt. Samia kwa wananchi wake.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Kasilda Mgeni wakati akifungua kikao maalumu kilichoandaliwa na Diwani wa Kata ya Same kwa lengo la kuwaeleza wazee hao masuala ya uchaguzi na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo Rais Dkt. Samia amefanya Kata na Wilaya ya Same.
“Jambo jema na la faraja kwetu wakazi wa Same ni kuona namna miradi ambayo tumepatiwa fedha na Rais Dkt. Samia inavyosaidia kubadili uchumi wa Wilaya yetu lakini pia mwananchi mmoja mmoja, katika hili kwa kweli mimi kama Mkuu wa Wilaya ya Same namshukuru sana mama Samia Same yetu sasa inazidi kusonga mbele kwa kasi”. Alisema Kasilda.
Aidha amesema kwa kutambua mchango wa wazee wa Same kwenye suala la uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika November 27 mwaka huu, amesisitiza pia wazee hao kukaa na familia zao kuwaeleza habari njema juu ya umuhimu wa uchaguzi huu ambao ndiyo unatoa dira ya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani wa mwaka 2025.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...