Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Agosti 8, 2024 ameongoza kikao cha Kamati Mahususi ya Kitaalamu ya Mawaziri wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) wanaoshughulikia masuala ya Afya, Lishe, idadi ya watu na udhibiti wa madawa.
Akiongea katika kikao hicho Waziri Ummy amesema kuwa atashirikiana vyema na uongozi wa AU na wanachama ili kuhakikisha majadiliano mazuri na utekekezaji wa mikakati mbalimbali ya kuboresha huduma za afya na Lishe barani Afrika inafanyika kikamilifu.
“Nchi za Afrika bado zina jukumu kubwa katika kuhakikisha jamii yetu inalindwa kwa kuelimishwa kuhusu masuala mbalimbali ya afya, lishe, uzazi wa mpango na udhibiti wa matumizi ya dawa za kulevya hususani kwa vijana pamoja na kudhibiti matumizi yasiyo sahihi ya dawa za binadamu”. Amesisitiza Waziri Ummy.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus ambaye pia aliudhuria kikao hicho
amesisitiza umuhimu wa kuimarisha upatikanaji wa bidhaa za afya pamoja udhibiti wa bidhaa hizo ikiwemo dawa.
“Natambua juhudi za AU katika kuanzishwa kwa Taasisi ya Udhibiti wa Dawa Afrika (AMA), chombo hicho kitumike katika udhibiti wa bidhaa za dawa na kuwejengea uwezo Mamlaka za udhibiti wa bidhaa za dawa katika nchi wanachama wa AU”. Amesema Dkt. Tedros.
Aidha, Waziri Ummy ameongoza Kikao hicho baada ya Tanzania kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Kiufundi ya Umoja wa Afrika ya Masuala ya Afya, Lishe, Idadi ya Watu na Udhibiti wa Dawa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...