Na Karama Kenyunko Michuzi Tv

WATUMISHI Housing Investiment (WHI) itafanya mkutano Mkuu wa kwanza wa mwaka Agosti 10 2024 Jijini Dar es Salaam wa mfuko wa uwekezaji wa Faida (Faida Fund), wakiyafikia mafanikio ya ongezeko la vipande vya thamani kwa asilimia 17 tangu kuanzishwa kwake mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 6,2024 Mkurugenzi mtendaji wa (WHI) Fred Msemwa amesema kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu mfuko huo umeanzishwa ukiwa na kiasi cha shilingi bilioni 12, na sasa ukiwa na kiasi cha Shilingi bilioni 27 kwa faida ambapo thamani ya vipande viliuzwa kwa shilingi 100 na sasa vinauzwa kwa shilingi 117 sawa na asilimia 17 ya ukuaji.

Amesema kuwa mkutano huo utakaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam utawapa fursa wanachama wake kujadili masuala mbalimbali yanayohusu mfuko huo.

“Katika kipindi cha muda mfupi mfuko wa Faida Fund umeweka misingi imara utakaoweza kuziba ombwe la wawekezaji wadogo la kushindwa kushiiriki kwenye masoko ya uwekezaji wa fedha ‘’ amesema Msemwa.

Amesema kuwa Faida Fund ndio mfuko pekee wa uwekezaji unatumia mfumo wa malipo ya serikali (GEPG) na kuwa na mifumo ya Tehama ambapo mwekezaji anaweza kujaza fomu au kuchota faida yake mtandaoni bila kufika ofisini.
 

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Watumishi Housing Investiment (WHI) Dkt. Fred Msemwa (katikati)  akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 6, 2024 jijini Dar es Salaam kuhusu Mkutano mkuu wa kwanza wa mwaka wa  Mfuko wa Uwekezaji wa Faida   (Faida Fund) unaotarajiwa kufanyika Agosti 10, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) uliopo jijini Dar es Salaam.
 

Meneja wa Biashara Benki ya CRDB, Msimamizi na Muangalizi wa Mfuko wa Uwekezaji wa Faida (Faida Fund) Marry Mponda  Kulia), akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 6, 2024 jijini Dar es Salaam kuhusu Mkutano mkuu wa kwanza wa mwaka wa Faida Fund unaotarajiwa kufanyika Agosti 10, 2024 katika Ukumbi wa Mikutano ya Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) uliopo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...