Alpha P amvuta Olamide kwenye ''W'', Mwimbaji wa Afrobeat kutokw nchini Nigeria Alpha P, amekuja kivingine kwa mashabiki zake kwa kuachia EP yake iitwayo ‘Welcome to the Pack’ ambayo ina ngoma tano. EP ya staa huyo itakupa hadithi ya kuvutia inayohusu kukatishwa tamaa, marafiki wa uongo, na vita zisivyoisha kwenye maisha. Katika EP hii producer Mkubwa Wondah, anahusika kuandaa kazi mbalimbali zinazopatikana hapo. EP inafunguliwa na ngoma ya “Light” ngoma ambayo inazungumzia namna anavyotafuta amani na furaha baada ya kufiwa na rafiki iliyebadilisha maisha yake, kisha inafuatiwa na wimbo wa mapenzi "W". Alpha P anaweka alama muhimu katika taaluma yake muziki kwa kushirikiana na rapa/mtunzi wa nyimbo na bosi wa lebo ya rekodi Olamide na mtayarishaji wa ThisIzLondon kupitia ngoma ya “W” ambayo anaenda kuwa mapinduzi makubwa ya burudani. Ngoma ya "Hold Ya" na "4 AM," ni ngoma mbili zinazoonyesha mtindo bora wa uandishi wa Alpha P.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...