Na Mwandishi Wetu.

BANK of Africa Tanzania , imeendesha semina kwa wajasiriamali wa Kahama mkoani Shinyanga , kupitia kauli mbiu ya “TUKUE PAMOJA” inayodhihirisha mkakati wake wa kusaidia wafanyabiashara wadogo na wa kati (SMEs) nchini Tanzania katika kufanikisha ukuaji wa kifedha na kuimarika kwa biashara zao.

Semina hiyo imefanyika hivi karibuni mjini Kahama na imelenga kutoa elimu ya kifedha kwa kina, ambapo mada mbalimbali za kibiashara zimefundishwa na kujadiliwa ikiwemo uwasilishaji wa rekodi za biashara, masuala ya kodi, na mikakati ya kuongeza uwezo wa huduma za kibenki ili kuchochea ukuaji wa mtaji.

Akiongea wakati wa ufunguzi wa semina hiyo, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa BOA benki, Hamza Cherkaoui amesema.... "katika mpango wetu wa kimkakati wa miaka mitatu, sekta hii nyeti ya wajasiriamali imepewa kipaumbele kwa njia ya kipekee, ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya kifedha kwa wateja wetu. Takwimu zinaonyesha kuwa sekta hii inachangia karibu asilimia 30 ya mapato ya taifa na katika biashara 10, 9 ni biashara zinazomilikiwa na wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati (SME), kati yao asilimia 54 ni Wanawake hivyo ni muhimu kuhakikisha tunawawezesha”.

Amesema, tangu kuanzishwa rasmi kwa programu hizo mwaka 2021, benki tayari imefikia wateja 500 wafanyabiashara wadogo wadogo (SME) na lengo la mwaka huu ni kufikia wateja 200.

"Matunda ya kile tunachofanya yanaonyeshwa katika matokeo mazuri tunayoshuhudia, ambapo faida ya benki imeongezeka kwa asilimia 33 kutoka Sh bilioni 6.03 hadi Sh.bilioni 9 kwa kulinganisha matokeo ya Juni mwaka jana na Juni mwaka huu." amesema Cherkaoui.

"Benki pia imeweza kupata matokeo mazuri katika mikopo chechefu, na katika kipindi kilichofikia Juni benki imefikia asilimia 1.5 ya mikopo chechefu, hii ni chini ya kiwango kinachohitajika na Benki Kuu ya Tanzania cha asilimia 5." Matokeo haya yanadhihirisha kuwa wateja wetu ni wazuri na wanalipa mikopo yao vizuri." Amesema.

Aidha, amewashukuru wateja wote wa BOA benki Tanzania kwa kuendelea kutuunga mkono na pia amewaomba wajasiriamali wa Tanzania, hasa wafanyabiashara wadogo wadogo na wa kati ((SME); benki iko tayari kuhakikisha mafanikio yao, kama kauli mbiu ya programu yeo "TUKUE PAMOJA" .

Naye, Kaimu Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa wateja wa reja reja (Retail Banking), Mwamvua Majeshi amewahakikishia wafanyabiashara kwamba huduma za mikopo zitatolewa kwa wakati bila kuchelewa kulingana na kanuni za kibenki hapa nchini. Pia watawapatia ushauri.

“Benki imefanikisha kutoa mikopo kwa biashara za kati (SMEs) yenye thamani ya shilingi bilioni 5 ikiwa imewanufaisha zaidi ya wafanyabiashara 2,000 wilayani Kahama hadi kufikia mwezi June mwaka huu”.

“Kwa hapa wateja wetu hupata huduma kupitia matawi yetu, hata hivyo, benki pia imewekeza katika huduma za kidijitali kama vile huduma za benki kwa simu (B-Mobile), huduma za benki za mtandao (BOAWeb-Internet Banking) na hivi karibuni tumezindua huduma ya Bank of Africa WAKALA yenye mawakala zaidi ya 200 nchini na hivi karibuni itakuja na huduma ya Lipa.” alisema Bi. Majeshi.

Baadhi ya wafanyabiashara waliohudhuria programu hiyo wameipongezakwa benki hiyo kwa jinsi ilivyo wawezesha kupitia mikopo na kuinua biashara zao na kuiomba benki hiyo iendelee kuboresha huduma zake ili kufaidisha Watanzania wengi
 

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Bank of Africa Tanzania, Hamza Cherkaoui, akizungumza na wateja wa benki hiyo waliohudhuria warsha  ya kuwajengea  uwezo iliyoandaliwa na benki hiyo  iliyofanyika Mjini Kahama mkoani Shinyanga hivi karibuni
 

 Mmoja wa Wateja wa Bank of Africa Tanzania Nzella Nzella, akichangia mada wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo wateja  wa Benki hiyo iliyofanyika mjini Kahama.
 

Mwezeshaji Erick Chrispin,  kutoka Taasisi ya True Maisha Consulting Group Ltd akitoa mada katika warsha ya kuwajengea uwezo wateja  wa Bank of Africa iliyoandaliwa na benki hiyo na kufanyika mjini Kahama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...