KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imepongeza juhudi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika kuboresha mitaala yake ili kukidhi mahitaji ya soko la ajira. 

Hayo yamebainishwa leo Septemba 10, 2024 Jijini Dar es  Salaam na kamati hiyo wakati ilipofanya ziara kwenye Chuo hicho kukagua utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya kiuchumi (HEET). 

Kamati hiyo ilibaini kwamba hatua hii ya kufanya mapitio ya mitaala imekuwa na mchango mkubwa katika kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira nchini.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Sekiboko amesema kwa muda mrefu ajira imekuwa kilio cha vijana licha ya kusoma elimu ya juu, hivyo tathmini ya aina hiyo ni muhimu ili kuhakikisha elimu inayotolewa ndiyo inahitajika kwenye soko la ajira.

"Kilichofanyika ni kizuri maana tusijifungie kwenye kutoa elimu bila kujifanyia tathmini kujua elimu inayotolewa inatatua changamoto zinazotuzunguka? Je mhitimu kwa ngazi ya chuo kikuu ana uwezo wa kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii.

“Tumefurahishwa pia na taarifa kwamba mnafanya tafiti ila tunachotaka matokeo ya tafiti hizi yawekewe wazo ili ziwe msaada kwenye jamii isiwe tafiti zinafanyika na kuishia kwenye makabati," amesema Mhe. Sekiboko.

Kwa upande wake Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo, Prof. Bernadeta Killian amesema tayari chuo hicho kimefanya mapitio ya mitalaa 60 kwa ngazi ya shahada ya kwanza na ya pili na iko katika hatua za mwisho kabla ya kuanza kutumika.

Aidha amesema utekelezaji wa mradi wa HEET katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, unahusisha ujenzi wa majengo mawili ambayo ni bweni lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40 na kukamilisha jengo la utawala na taaluma.

Amesema jengo la utawala na taaluma litakuwa na madarasa manne yenye uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi 216, ukumbi wa mikutano wenye uwezo wa kuchukua watu 150, ofisi ya wafanyakazi, na maabara tano.

Pamoja na hayo Prof. Killian amesema ujenzi wa majengo mbalimbali ya mradi ulianza Februari ,2024 na utakamilika baada ya miezi 18 na utagharimu kiasi cha Tsh. 11, 194,677,531.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mhe. Husna Juma Sekiboko akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo pamoja na Menejimenti ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara kutembelea utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) leo Septemba 10, 2024 katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ilipofanya ziara kukagua utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Septemba 10, 2024.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo, Prof. Bernadeta Killian akizungumza wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo ilipofanya ziara kukagua utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) katika Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Septemba 10, 2024.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mhe. Husna Juma Sekiboko, (mwenye ushungi) akiongozana na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo, Prof. Bernadeta Killian pamoja na Wajumbe wa Kamati wakati walipofanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, Mhe. Husna Juma Sekiboko, (mwenye ushungi) akiongozana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga,Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo, Prof. Bernadeta Killian pamoja na Wajumbe wa Kamati wakati walipofanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Juma Sekiboko wakikagua mradi wa ujenzi wa jengo la Taaluma na Utawala unaotekelezwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) wakati walipofanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Juma Sekiboko wakikagua mradi wa ujenzi wa jengo la Taaluma na Utawala unaotekelezwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) wakati walipofanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.
Ujenzi wa engo la Taaluma na Utawala ukiendelea katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Omary Kipanga akizungumza jambo na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo-Mipango, Fedha na Utawala, ambaye pia ni Mratibu wa mradi huo, Prof. Bernadeta Killian wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Juma Sekiboko kufanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Husna Juma Sekiboko wakikagua mradi wa ujenzi wa bweni unaotekelezwa kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET) wakati walipofanya ziara katika Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu visiwani Zanzibar Septemba 9,2024.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...