Na WAF - Dar Es Salaam 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amewataka Watanzania kuchangamkia fursa za kupata huduma bora za Afya ikiwemo kupandikiza mimba zinazotolewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. 

Dkt. Mpango amesema hayo leo Septemba 11, 2024 baada ya kuzindia kitua cha upandikizaji mimba (IVF) cha Dkt. Samia Suluhu Hassan, gari la huduma tembezi za Afya (Mobile Medical Services) pamoja na kuwasha vifaa vya kusaidia kusikia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam. 

"Ninawasisi Watanzania wenzangu sasa tuchangamkie fursa zinazotolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili, huduma ambazo ni bora na zenye gharama nafuu ikiwemo huduma za kibingwa kama huduma hizi za upandikizaji mimba." Amesema Dkt. Mpango 

Aidha, Makamu wa Rais Dkt. Mpango amewataka watumishi kuvitunza vifaa hivyo ili viendelee kutoa huduma kwa wananchi kama ilivyokusudiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Afya.

Amesema, Serikali inaendelea kuchukua jitihada za kuboresha Sekta ya Afya ikiwemo kuendeleza mpango wa kuwajengea uwezo wataalamu wa ndani kujua kutumia vifaa hivyo na kuwahudumia Watanzania ili kuondokana na utegemezi wa wataalamu kutoka nje ya nchi. 
Kwa upande wake Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amevitaka vituo vya Afya vyote nchini, pamoja na Hospitali kuweka kipaumbele katika tiba na kuokoa uhai wa wananchi kwa kuwa hivyo ni vipaumbele vya Serikali. 

"Mhe. Mkuu wa Mkoa ameeleza hapa changamoto za utoaji maiti, tunaendelea kusema huduma bora za Afya liwe jambo la msingi na kuhakikisha kwamba kila anaepata changamoto na kukamilisha taratibu tulizoziweka ahudumiwe haraka, iwe ni kutoa maiti au huduma nyingine, maswala miengine baadae." Amesisitiza Waziri Mhagama

Amesema, Serikali kupitia Wizara ya Afya inatengeneza mifumo itakayosomana ili kupunguza gharama kwa wananchi ambapo mgonjwa anaweza kutibiwa akiwa katika Hospitali ya yoyote ya Mkoa akapata vipimo na akienda Hospitali ya Taifa anaendelea pale alipoishia kwa kiwa mifumo itakua inasomana. 

"Tunamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha ili kuhakikisha Watanzania ambao hawana uwezo wa kulipia huduma za Afya, tunapoelekea kwenye Bima ya Afya kwa wote nao waweze kupata huduma bila kikwazo cha fedha." Amesema Waziri Mhagama






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...