MFUKO wa Uwekezaji wa Pamoja wa Alpha Halal Fund umeingia makubaliano na kampuni tanzu ya soko la hisa la Uingereza, Infinitive, kwa ajili ya kupata taarifa muhimu za masoko duniani.
Akizungumza katika hafla hiyo leo Septemba 7,2024 Jijini Dar es Salaam Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Alpha Halal Fund Gerase Kamugisha, akieleza kwamba Refinitiv, itatoa huduma muhimu katika kuchambua na kutathmini bidhaa na kampuni zinazohusiana na masoko duniani.
"Kampuni hii inajulikana kwa uwezo wake wa kutoa taarifa kuhusu kampuni zinazozingatia sheria za halal na zile zisizozingatia".
Kamugisha alisema, "Refinitiv itatusaidia kupata taarifa muhimu kuhusu bidhaa na kampuni zinazohusiana na masoko duniani. Hii itatusaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu wapi tunaweza kuwekeza ili kupata faida nzuri."
Aliongeza kwamba baada ya kupata na kuchambua taarifa kutoka Refinitiv, Afisa Msimamizi wa Sheria wa Alpha Halal Fund atashirikishwa katika mchakato wa kufanya maamuzi, kuhakikisha kwamba uwekezaji unafanywa kwa kuzingatia kanuni za kisheria na kimaadili.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...