WAKULIMAwa Wilaya ya Namtumbo wameimba kwa nderemo na vifijo kwa kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwaletea wakulima, huku Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe (Mb) akiwasihi kuendelea kuleta tija ili kunufaika na neema hiyo. 

“Sisi wakulima tunampompigia kura Mhe. Rais Samia ni kwa sababu amekuwa Rais aliyegusa maisha yetu. Huyu ndiye Rais ambaye amekuja madarakanj anampa ruzuku Mkulima kuanzia shambani hadi sokoni, kwa maana mbegu, mbolea na ata zana za kilimo,” amesema Waziri Bashe.  

Waziri Bashe amesema hayo akiwa katika mwendelezo wa ziara yake mkoani Ruvuma katika eneo la Rwinga, Wilaya ya Namtumbo tarehe 21 Septemba 2024. 

Aidha, ametatua mgogoro wa ardhi inayomilikiwa na Serikali chini ya Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) ambapo hapo nyuma alipatiwa mwekezaji kampuni ya NAFCO kuwekeza.  Hata hivyo, mwekezaji huyo akatokomea na Serikali kulichukua shamba, ambalp wananchi waliliendeleza.  

“Niwashukuru wananchi kwa kuendeleza shamba hilo na kupitia mhadhara huu “tuchimbe ngoko” kama wanavyosema wasukuma ili tuweke mambo sawa,” amesema Waziri Bashe.  Ameelekeza wakulima wagaiwe ekari 3000 na zilizobaki 3580 Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA) atumie kulima mbegu bora, kuweka mashine ya kısasa ya kusafisha mbegu na ghala la kuhifadhia mbegu.

Ziara ya Namtumbo pia imewashirikisha Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe. Ngollo Malenya, Mhe. Vita Kawawa, Mbunge wa Jimbo la Namtumbo, viongozi mbalimbali kutoka Wizarani, Taasisi za Wizara, Serikali ya Mkoa na Wilaya, na Chama cha Mapinduzi.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...