KUPITIA Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) inatekeleza mradi wa EASTRIP (East Africa Skills for Transformation and Regional Integration Project) ambao ujenzi wake uko mbioni kukamilika unadhamiria kuimarisha ustadi wa kiufundi na kitaaluma ili kuchochea maendeleo ya viwanda na mabadiliko ya uchumi katika nchi husika.

Mradi wa EASTRIP ni mradi wa kikanda unaotekelezwa katika nchi za Tanzania, Ethiopia, na Kenya. Lengo kuu la mradi huu ni kuanzisha vituo vya umahiri katika maeneo ya ujuzi muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi ya mataifa hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 13, 2024 Jijini Dar es Salaam, mara baada ya kufanya ziara ya kutembelea mradi wa EASTRIP katika Chuo hicho, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Sylvia Lupembe amesema mradi huo unahusisha ujenzi wa majengo matano, ambayo ni Majengo mawili ya mabweni ya wanafunzi (hostels); jengo ambalo litakuwa na madarasa pamoja na ofisi (center of excellence building), jengo litakalojumuisha karakana za mafunzo (high tech building), maabara (lab workshops), kituo cha mafunzo kwa ndege (aircraft simulator) na maabara nane za kompyuta.

"Majengo haya yatasaidia kuimarisha uwezo wa Chuo cha Usafirishaji katika kutoa mafunzo ya kiwango cha juu kwa wataalamu wa usafirishaji na teknolojia zinazohusiana na sekta hiyo". Amesema Sylvia.

Aidha Sylvia amesema Wizara imejidhatiti kuongeza ubora wa elimu kwa kuhakikisha kuwa vijana wanaozalishwa wanakuwa na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira na vilevile unaoendana na mabadiliko ya kiteknolojia









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...