MNADHIMU Mkuu wa JWTZ Luteni Jenerali Salum Haji Othuman ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi na Mambo ya Nje ya Kisiwa cha Ushelisheli kwa kuthamini mchango mkubwa uliotolewa na JWTZ katika harakati za ukombozi barani Afrika.
Luteni Jenerali Othuman ameyasema hayo alipotembelewa na kamati hiyo Makao Makuu ya JWTZ Msalato jijiji Dodoma tarehe 03 Septemba 2024.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Francois Adelaide amesema JWTZ limekuwa msaada mkubwa sana kwa nchi nyingi za kusini kwa Afrika.
Amesema nchi yake itaendelea kukuza diplomasia ya Ulinzi hasa kwenye mafunzo, mazoezi pamoja na kubadilishana ujuzi katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kukabiliana na majanga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...