MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imewaagiza wamiliki wote wa vituo vya mafuta ya petroli nchini kuhakikisha wanachukua hatua stahiki zinazozingatia usalama wa afya, mali na mazingira wakati wote wa uendeshaji wa biashara hizo.

EWURA imetoa agizo hilo kutokana na ongezeko la matukio ya milipuko ya moto inayotokana na uhifadhi au uuzaji holela wa mafuta ya petroli kwa kutumia madumu au chupa jambo kinyume na tahadhari za usalama wa afya, mali na mazingira (HSE).

Taarifa iliyotolewa Septemba 16, 2024 na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile, imewasisitiza wafanyabiashara ya vituo vya mafuta nchini kutoruhusu uuzwaji wa mafuta katika vifaa visivyoruhusiwa kuchukulia au kubebea mafuta ya petroli kama vile madumu, chupa aina zote na vifaa vingine visivyoruhusiwa kisheria.

"Tunawahimiza wamiliki wa vituo vya mafuta kuepuka vitendo vinavyoweza kuhatarisha maisha ya watu, mali, na mazingira wakati wa uendeshaji wa biashara zao na kuchukua tahadhari stahiki kwa kuzingatia matakwa ya Kanuni ya 27 ya Kanuni zinasimamia biashara ya vituo vya mafuta nchini”.

Pia, EWURA imebainisha kuwa, itaendelea kufanya ukaguzi wa kina kwenye vituo vya mafuta kote nchini ili kuhakikisha utekelezwaji wa kanuni hizo, na yeyote atakayekiuka hatua kali za kisheria ziatachukuliwa dhidi yake ikiwemo kufungiwa vituo vyao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...