Raisa Said, Tanga
MKUU wa Mkoa wa Tanga Balozi Dkt Batilda Buriani ameitaka Hospital ya rufaa ya mkoa Bombo kuwa ya mfano kwa kuchukua tahadhari ya kujikinga na na ugonjwa wa Homa ya nyani 'Mpox' ambao licha ya kutokuwepo hapa nchini bado tahadhari ni lazima zichukuliwe ili kujiweka tayari Kupambana kabla na baada ya kutoka.
Dkt Buriani ameota Rai hiyo wakati alipofanya ziara ya kukagua na kutembelea maendeleo ya miradi mbalimbali inayotekelezwa katika hospital hiyo kwa lengo la kuboresha utoaji wa huduma ambapo pia kamati ya usalama ya mkoa ilikabidhi bango linaloonyesha tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo huku akigiza jitihada zilizofanyika wakati wa janga la COVID-19 zifanyike ili kujikinga.
Amesema kuwa ugonjwa huo ambao kwa sasa umesharipotiwa katika nchi za Kenya ,Uganda pamoja na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ni lazima tahadhari zichukuliwe ikizingatiwa kuwa Mkoa wa Tanga upo jirani pamoja na muingiliano wa watu kutoka Kenya wanaokuja Tanzania katika nyanja mbalimbali ikiwemo za kibiashara.
"Tuna changamoto ya homa ya nyani 'Mpox' tulifikiri katika hospital ya kwqnza kabisa ya mkoa ndio muwe kielelezo sijaona hata mabango mliyoyaweka ya kuonyesha tahadhari ya Empox, sasa hivi kama Empox ipo Kenya ,Uganda, Congo kufika Tanzania sio shida tutaweza tu kuokoka kama tutazingatia masharti ya kujikinga na ugonjwa huu ikiwemo maswala ya kurudi kule tulikofanya wakati wa COVID-19 kuweza kunawa mikono kwa maji tiririka na kutokushikana mikono ili kuepukana na ugonjwa huu" amesema Dkt Buriani
"Sisi kama kamati ya usalama ya mkoa tumekuja na kielelezo tusisubiri mpaka wizara ituambie cha kufanya , sisi wenyewe tuonyeshe utayari na nyinyi wenyewe kama mkionyesha wa wilaya vituo vya afya na Zahanati wataiga kila mtu ataenda kuhakikisha hili janga linasimamiwa" alisisitiza.
Aidha Balozi Buriani amesema kutokana na uwepo wa ugonjwa wa kipindipindu ulioibuka katika wilaya ya Kilindi ambapo wagonjwa 88 waliripotiwa zilifanyika jitihada za makusudi ikiwepo timu ya wataalam kuweka Kambi ambapo ilifanikiwa kupunguza maambukizi hayo hulu Serikali ikiendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuhakikisha inabiresha huduma ya upatikanaji wa maji safi na salama.
"Tuna changamoto ya kipindipindu kinaendelea kuisha na sasa kipo kwenye wilaya yetu ya Kilindi tulikuwa tuna wagonjwa 88 ndani ya wiki moja tuliagiza wataalamu waweke Kambi wahakikishe kwamba kusiyokee mgonjwa mwingine tena na sasa leo (Juzi) nimeambiwa amebaki mgonjwa mmoja.
hii imetokana na vyanzo vya maji kutokuwa salama wenzetu wa Kilindi wanategemea sana maji ya Kisima na chem chem tunayo miradi mikubwa ya maji ambayo inaendelea kukamilishwa mpaka ikifika mwakani tutakuwa tumefikia asilimia 95 ya miradi iliyokamilika mjini na vijijini itakuwa ni 85 na sasa hivi wastani wa upatikanaji wa maji katika Mkoa wetu ni asilimia 56 na maen o kama ya Handeni Kilindi bado ipo chini ya asilimia 40 kwahiyo ikitokea changamoto kama hii ya kipindipindu ni lazima tufanye jitihada zote tupate madawa ya kuhakikisha tunasafisha yale maji ili mtu ambaye atashindwa kuchemsha awe anapata maji ambayo yameshasafishwa kupitia zile na hicho ndicho tulichokifanya kupitia kwa mganga Mkuu wa Mkoa lakini tunaendelea kuboresha upatikanaji wa maji katika maeneo yetu ya Handeni ili kipindipindu kisiendelee kusambaa"
Aidha Dkt Buriani ameipongeza Hospital hiyo kwa kuendelea kutoka huduma kwa wagonjwa licha ya baadhi yao kukosa fedha za matibabu ambapo mpango uliopo sasa ni kuhakikisha wagonjwa wote wanaogika hospitalni hapo wanapatiwa huduma huku wakie delea kulipa kidogo kidogo mpaka deni litakapoisha.
Mkuu wa mkoa huyo ameutaka uongozi wa hospital hiyo kuwasiliana na uongozi wa Jiji la Tanga kuweka mkakati wa pamoja katika kuhakikisha usalama wa afya kwa wananchi wanaofika kupata huduma katika hospital hiyo unakuwepo wakati wote hii ikiwa ni njia ya kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na mahonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindipindu na homa ya nyani.
"Uongozi wa jiji la Tanga pamoja na hospital kuona hali nzima ya shughuli zinazoendelea nje ya hospital kuweza na usimamizi nzuri pamoja na uwepo wa maji tiririka ili hospital iendelee kuwa katika mazingira mazuri kwa sababu katika hali ya sasa hivi hospital yetu ni chafu taka kila Kona ni lazima kuhakikisha kwamba mazingira ya hospital yetu ya nakuwa Bora na ya kuridhisha
Awali akizungumza mganga mfawidhi wa hospital ya rufaa ya mkoa Bombo amesema kuwa ipo miradi mbalimbali inayotekelezwa katika hospital hiyo ikiwemo ukarabati wa majengo ya kutolewa huduma ikiwemo jengo la idara ya macho, jengo la mazoezi, jengo la kuhifadhia maiti , ambayo yote yanahitaji ukarabati kutokana naiundombinu yake kuwa ya muda mrefu.
Amesema pamoja na ujenzi wa majengo mbalimbali yanayojengwa ni pamoja na jengo la damu salama ambalo litagharimu kiasi cha billion 2 linalojengwa kwa awamu mbili , mradi wa jengo la wodi binafsi ambao utagharimu shilingi Milion 199 ambapo tayari makandarasi ameshalipwa shilingi Milion 87 na ujenzi .
Amesema kwa wastani hospital hiyo imekuwa ikipokea wagonjwa wengi wa magonjwa yasiyoambukiza hususani shinikizo la juu la damu pamoja na kisukari wakifwatiwa na wagonjwa wengine wakiwemo wa ajali.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...