Na WAF - Dodoma
Waziri wa Afya Mhe. Jenister Mhagama amelitaka Baraza la Madaktari Tanganyika kujipanga zaidi ili kuendana na kasi ya mabadiliko makubwa ndani ya Sekta ya Afya yanayotokea na uongozi mahiri wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
"Waziri Mhagama ametoa wito huo leo Septemba 05, 2024 kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Afya na Masuala ya UKIMWI ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Elibariki Kingu (Mb) kwenye kumbi za Bunge Jijini Dodoma.
“Sekta ya Afya imekuwa sana, na hivi sasa kuna Ultrasound ya Jicho kitu ambazo zamani hakikuwepo na ukipata tatizo unatakiwa uende India, hivyo wanataaluma wanatakiwa waendele kujifunza hususani kwenye matumizi ya vifaa na kukakikisha huduma hizi zinawafikia wananchi wote hasa wa vijijini." Amesema Waziri Mhagama
Kwa upande wake msajili wa Baraza la Madaktari Tanganyika Dkt. David Mnzava, amesema mpaka sasa Baraza limefanikiwa kuwasajili wanataaluma Zaidi ya 9,983 kwa kipindi cha mwaka Mmoja pekee.
“Hadi Juni 30 2024 Jumla ya wanataalamu 9,983 wamesajiliwa kufikia idadi ya wataalamu 41,937 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 31.” Amesema Dkt. Mnzava
Dtk. Mnzava amesema ongezeko hilo litakwenda kuongeza utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...