WAKAZI wanaoishi Kata za Kilosa na Mbambabay, na Kijiji cha Ndesule kujengewa skimu ya umwagiliaji itakayoitwa Kimbande (jina linalotokana na maeneo hayo matatu).

Hayo yamesemwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe (Mb) tarehe 20 Septemba 2024, Wilayani Nyasa ambaye aliambatana na Mhe. Eng. Stella Manyanya, Mbunge wa Nyasa na Mhe. Peres Magiri, Mkuu wa Wilaya ya Nyasa ambao walitaka kumuonesha uhitaji wa skimu hiyo kwa wakazi hao.

“Nailekeza Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kuanza ujenzi wa skimu ya Kimbande ambayo Ina ekari 750 za kilimo cha mpunga. Ujenzi uwe na awamu mbili, kutengenezwe kingo za maji ili yabaki kwenye mto; na pili kuwe na sehemu ya kukusanya maji ili yawe juu kama mabwawa,” amesema Waziri Bashe.

Ameomba wakulima na wafugaji waliopo pembezoni mwa mto Makata kutoa ushirikiano na kupisha ujenzi wa skimu pale kazi itakapoanza.

Waziri Bashe yupo katika ziara ya kikazi katika kuleta maendeleo kwa wakazi wa Mkoa wa Ruvuma kuanzia tarehe 17 hadi 24 Septemba 2024.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...