Na Mwandishi Wetu, Michuzi Blog
KATIKA kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, ALAF Limited, kampuni inayotoa huduma za ujenzi, imefungua showroom mpya katika mji wa Tunduma, Mkoa wa Songwe ili kwasogezea karibu huduma wateja wao.
Hii ni hatua inayothibitisha dhamira ya ALAF ya kutoa huduma bora na kukidhi mahitaji ya wateja hususani Mji wa Tunduma na maeneo ya jirani.
Showroom ya Tunduma imefunguliwa wakati ambapo mji unakua kwa kasi, ukichochewa na miradi mingi ya maendeleo na uwepo wake katika eneo la mpaka wa Tanzania na Zambia.
Kituo hiki kipya kitakuwa rasilimali muhimu kwa wakaazi na wafanyabiashara, kuwapa fursa ya kupata suluhisho za ujenzi zenye ubora wa hali ya juu kutoka ALAF bila usumbufu wa kusafiri umbali mrefu.
Akizungumuza wakati wa uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Daniel Chongolo, ameipongeza ALAF kwa hatua hiyo muhimu, akisisitiza kwamba inaonyesha kujitolea kwa kampuni katika kuridhisha wateja.
“Ufunguzi wa showroom hii wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja unaonyesha dhamira ya ALAF katika kuimarisha utoaji wa huduma kwa wakazi wa Tunduma, Mpango utakaosaidia kuokoa muda na kuwawezesha kupata suluhisho bora la ujenzi kwa urahisi,”.
Aidha Chongolo ametoa wito kwa wakazi wa Tunduma na wafanyabiashara kutumia fursa hiyo kupata ufumbuzi sahihi wa mahitaji ya bidhaa za ujenzi na thamani ya fedha kwani ALAF inajulikana kwa utoaji wa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu.
Amesema kwamba wakazi wa Tunduma hawana sababu ya kujenga nyumba na majengo yasiyo bora wakati ALAF iko karibu nao na inatoa bidhaa bora.
"Kama serikali, tutaendelea kuwasaidia wawekezaji wote wa Tunduma, ikiwa ni pamoja na ALAF, kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara ili waweze kupata faida na uwekezaji," alisisitiza.
Kwa upande wake, msimamizi Mkuu wa Matawi ya ALAF, Naeema Abdul amesema... “Tuna furaha kubwa kuzindua showroom yetu wakati wa Wiki ya Huduma kwa Wateja, ambayo ni uthibitisho wa mkazo wetu katika kutoa huduma bora. Nafasi hii mpya itatuwezesha kuelewa mahitaji ya wateja wetu na kuwapa suluhisho kwa wakati."
Kwa mujibu wa msimamizi huyo, ALAF imeitikia wito wa muda mrefu kuwekeza Tunduma ili kukidhi mahitaji ya wateja.
“Sisi ni kampuni inayoongoza kwa kutoa suluhishi bora za ujenzi nchini Tanzania, Tunataka kuwahakikishia wakazi wa Tunduma kwamba tuna bidhaa na huduma bora zitakazowapa thamani halisi ya fedha zao,” amesema.
Uzinduzi huo wa showroom ulihudhuriwa na viongozi na wadau mbalimbali ndani ya Mkoa wa Songwe, ambao walipata fursa ya kuona bidhaa za ALAF na kuonana na uongozi na wafanyakazi wa ALAF.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...