Raisa Said, Tanga

Rasmi, Hatifungani ya Kijani ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Tanga (Tanga UWASA) yaorodheshwa katika Soko la Hisa la nchini Luxembourg.

Tukio hilo limeshuhudiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Maji Eng. Mwajuma Waziri, viongozi mbalimbali wa Wizara ya Maji, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na baadhi wa wajumbe wa Menejimenti ya TangaUWASA, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, pamoja na uwakilishi kutoka CMSA na UNCDF.

Hatifungani ya Kijani ya TangaUWASA yenye thamani ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 53.12 ambayo imelenga kuboresha hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira kwa wananchi inakuwa ni Hatifungani ya kwanza Afrika Mashariki kuorodheshwa katika soko la hisa nchini Luxembourg.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...