KLABU ya Manchester United inachechemea kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza ambayo mpaka sasa imeshachezwa michezo saba kunako ligi hiyo pendwa kabisa ulimwenguni.

Klabu hiyo ambayo msimu huu ilifanya usajili mzuri kuelekea kuanza kwa msimu na matarajio yakiwa makubwa kwa klabu hiyo, Lakini mambo yamekua tofauti kwani timu hiyo imefanya vibaya sana mpaka sasa na mpaka kufikia hatua ya kufikiria kufukuza kocha.

Manchester United mpaka sasa sasa wamekusanya alama nane tu kwenye michezo saba ambayo wamecheza kwenye ligi kuu ya Uingereza ukiwa wastani mbovu zaidi kwa miaka ya hivi karibuni, Hali hii inaendelea kuzua sintofahamu kwa klabu hiyo na hali ya kibarua cha kocha Erik Ten Hag.

Wahafidhina mbalimbali wanaamini kocha wa klabu hiyo Erik Ten Hag hatoshi ndani ya klabu hiyo na ni muda sahihi sasa wa kuonyeshwa mlango wa kutokea kutokana na mwenendo wa timu hiyo ambao wamekua nao msimu huu.

Endelea kufurahia kubashiri na Meridianbet mabingwa wa michezo ya kubashiri ambao wanatoa ODDS BOMBA kuliko mahala pengine, Lakini pia machaguzi mengi zaidi ya 1000 Bashiri sasa michezo itakayopigwa wikiendi hii uweze kupiga mkwanja.

Lawama nyingi sana zinamuendea kocha Ten Hag kutokana na muda ambao amehudumu klabuni hapo mpaka sasa, Lakini pia sajili ambazo amezifanya kwa kiasi kikubwa ikionekana ni mapendekezo yake lakini mabadiliko yamekua hafifu mno jambo ambalo limefanya mashabiki kuona ni muda sasa Mholanzi huyo atimke.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...