■Maboresho makubwa ya Miundombinu ya Utalii yaja

Na Happiness Shayo

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi,Dkt. Pindi Chana (Mb) amezindua rasmi utalii wa puto ikiwa ni Maadhimisho ya Miaka 60 ya Hifadhi ya Taifa Ruaha.

Uzinduzi huo umefanyika leo Oktoba 7,2024 katika eneo la Korongo View ndani ya Hifadhi ya Taifa Ruaha Mkoani Iringa.

Akizungumza katika mahojiano maalum ya Kipindi cha Jambo Tanzania ya Shirika la Utangazaji la TBC, Mhe. Chana amesema mafanikio hayo ni kutokana na jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii.

"Tunamshukuru Rais Samia kwa kuionesha dunia vivutio vya utalii vya Tanzania ambapo mpaka sasa watalii wameongezeka na kufikia milioni 1.8 na mapato ya Taifa tunachangia asilimia 17% na fedha za kigeni takribani dola za kimarekani Bilioni 3.6.

Kuhusu maboresho ya
Miundombinu katika Hifadhi ya Taifa Ruaha Mhe. Chana amefafanua kuwa mpaka sasa kuna barabara ya Iringa- Msembe yenye urefu wa kilomita 104 ambayo inaenda kujengwa.

Aidha, amesema katika Hifadhi ya Taifa Ruaha kutakuwa na uwanja wa ndege sambamba na kutumia uwanja wa ndege wa Nduli uliopo Mkoa wa Iringa ambao unaendelea kukarabatiwa.

Amesema ndani ya miaka 3 kumekuwa na mabadiliko makubwa ya sekta ya utalii na Serikali inazidi kuboresha maeneo mengi ya Utalii huku akihamasisha wawekezaji kujitokeza kuwekeza katika hifadhi hiyo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...