Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo akizungumza wakati wa kupokea taarifa ya mapitio ya rasimu ya Dira ya Taifa 2050.




WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Mhe. Profesa Kitila Mkumbo (Mb), amepokea Taarifa ya Mapitio ya Rasmu ya Dira 2050 kutoka kwa wajumbe wa timu ya mapitio ya rasmu hiyo.
Kikao hicho muhimu baina ya Mhe Prof. Mkumbo na Timu ya Mapitio ya Rasmu ya Dira 2050, kilichohudhuriwa na Katibu Mkuu Dkt. Tausi Kida Mbaga, kimelenga kuboresha rasmu ya Dira 2050 kupitia mapendekezo ya timu hiyo.
Aidha, timu ya mapitio ya rasmu ya Dira 2050 imezingatia ushirikishwaji mpana wa wadau kutoka sekta za umma, binafsi na asasi za kiraia.
Baada ya kupokea taarifa ya mapitio, Mheshiwa Waziri Prof. Mkumbo amewashukuru wajumbe wa timu ya mapitio kwa kazi kubwa waliyoifanya na kuiagiza timu kuu ya uandishi wa Dira kuzingatia mapendekezo yote yaliyotolewa na kuchukua hatua zinazofaa kuzalisha rasmu ya Dira 2050 yenye viwango vya juu vya ubora.
Vile vile, Mheshimiwa Prof. Mkumbo amewasihi wajumbe wa timu ya Mapitio ya Rasmu ya Dira 2050 kuendelea kutoa ushirikiano kwa Timu Kuu ya Uandishi wa Dira 2050 ili kutoa ufafanuzi zaidi juu ya mapendekezo waliyotoa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...