Na Linda Akyoo -Arusha
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Doto Mashaka Biteko leo Oktoba 09, 2024 amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda kwa ubunifu wake katika Uongozi, suala ambalo limechangia kuitangaza Arusha kimataifa na kuvutia wageni na mikutano mingi zaidi kwenye Mkoa huo wa Kaskazini mwa Tanzania.
Akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Mkutano wa Mwaka wa Wataalamu wa Mionzi kutoka barani Afrika kwenye Kituo cha kimataifa cha mikutano cha AICC Jijini Arusha, Naibu Waziri Mkuu amesifu pia mapokezi mazuri wanayoyapata wageni na Viongozi mbalimbali wanapokuja Arusha kwaajili ya shughuli mbalimbali na kusema ugeni huo umesaidia pakubwa kusisimua uchumi wa Mkoa wa Arusha.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...