-Katika kuchochea uandishi wa habari za maendeleo

Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) wameandaa Tuzo ya Samia Kalamu 'Samia Kalamu Awads ' kwa Waandishi wa habari kuandika habari za maendeleo katika nyanja mbalimbali.

Kauli mbiu ya Tuzo hizo ni Uzalendo ndio Ujanja zikiwa na lengo la kuchochea uandishi wa makala zilizofanyiwa utafitib kuhusu maendeleo, uwajibikaji, uzalendo na kujenga chapa na taswira ya nchi ya Taifa.

Akizungumza wakati wa kutangaza tuzo hizo, Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Dkt. Rose Reuben amesema tuzo zitahusisha maudhui yaliyochapishwa kupitia magazeti, Radio, Televisheni, Majukwaa ya mtandaoni pamoja Maafisa habari wa serikali.

"Tuzo hizi zilizoandaliwa na TAMWA na TCRA zitahusisha habari zilizochapishwa kati ya Januari 1 hadi Oktoba 26,2024.

Tuzo ni kuhamasisha, kuhimiza na kukuza wigo wa uchakataji, utangazaji na uchapishaji maudhui ya ndani kupitia vyombo vya habari",amesema Dkt. Rose.

"Kutokana na maendeleo ya teknolojia na utandawazi, uandishi wa habari nchini umekuwa ukijikita kwenye kuburudisha, kuhabarisha huku uandishi wa makala za kuelimisha zikiwa kwa kiwango kidogo lakini pia vyombo vya habari nchini vimekuwa vikitangaza maudhui ya nje yasiyokidhi mahitaji ya hadhira ya Kitanzania.

Amesema kutokana na kuwepo katika sintofahamu hiyo TAMWA kwa kushirikiana na TCRA waliamua kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari, watangazaji , Wahariri,Mameneja, Maafisa Habari, Wamiliki wa vyombo vya habari, Wahadhiri na watengeneza maudhui wa mitandaoni wapatao 2,054 kote nchini kwa kipindi cha miezi mitatu mwaka huu 2024.

Hata hivyo amesema pamoja na mafunzo hayo wameona ni vyema kutoa tuzo kwa wanahabari pamoja na vyombo vya habari ambao wamekuwa wakifanya jitihada za kuandika, kuchapisha na kutangaza maudhui ya ndani hasa makala zilizofanyiwa utafiti na uchambuzi wenye tija kwa watanzania.

"Tuzo hizi zimepewa jina la Samia Kalamu Awards ili kutambua na kuenzi historia ya kupata Rais wa kwanza mwanamke nchini Tanzania.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Novemba 2024 zikiwa katika makundi matatu ambayo ni Tuzo Maalum za kitaifa, Tuzo kwa vyombo vya habari na Tuzo za Kisekta.

Vigezo vya ushiriki kuwa ni Makala zinazoshindanishwa ziwe zinahusu masuala ya maendeleo yanayogusa maisha ya wananchi na fursa zinazopatikana kutoka kwenye miradi mbalimbali iliyotekelezwa na kuwa na vyanzo vinne katika makala hizo

Amesema Makala hizo ziwe zimechapishwa, kutangazwa au kurushwa kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza kwenye vyombo vya habari vya ndani au nje ya Tanzania.

Aidha mwandishi awe Mtanzania na makala iwe imefanyiwa utafiti na uchambuzi wa kina. Vyanz vya habari visipungue vinne na makala hazipaswi kuwa zimeshawahi kushindanishwa kwenye tuzo nyingine.

Amesema kwa kuzingatia ulinzi wa haki miliki, kazi zote zitakazowasilishwa kwa ajili ya mashindano ni lazima ziwe za kipekee na zifuate masharti ya hakimiliki ya mwandishi na kituo kilichotangaza.

Dkt. Rose amesema mchakato wa upigaji kura utahusisha wananchi kwa asilimia 60 na majaji kwa asilimia 40, kura zitapigwa kupitia SMS SHORT CODE namba 15200 kupitia simu na kutumia tovuti ya https://samiaawards.tz kwa mawasiliano zaidi tembelea tovuti https://samiaawards.tz

Amesema matarajio ya tuzo za Samia Kalamu Awards zitahamasisha uandishi wa habari unaozingatia weledi, maadili, kukuza maendeleo ya Tanzania na uzalendo hivyo kila mwanahabari anatakiwa kutumia fursa hii kuwasilisha kazi kupitia tovuti ,https://samiaawards.tz.

Meneja Huduma za Utangazaji TCRA, Mhandisi Andrew Kisaka akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari amesema lengo la tuzo hizo pia ni kuhakikisha waandishi wa habari wanaandika makala zenye maudhui bora na zenye kuleta mabadiliko.

“ Tuzo hizi ni za kipekee kwa sababu vyombo vya habari vyote vitashindishwa, maafisa habari nao watashindanishwa hivyo ni chachu kwa vyombo vya habari na waandishi wa habari kufanya kazi kwa weledi zaidi. Zitaleta matokeo chanya katika tasnia ya habari.

"Tunahitaji waandishi wa habari wanaoandika habari zenye kuleta mabadiliko lengo ni kuongeza kiwango bora cha maudhui ya ndani.amesema Mhandisi Kisaka

Washindi wa Tuzo hizo ni fedha Cheti pamoja vifaa vya kazi ambapo waandishi wa habari watapata.
 

Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA Dkt. Rose Reuben akizungumza wakati wa kutangaza  Mashindano ya Tuzo za Waandishi wa habari za maendeleo 'Samia Kalamu Awards'  zenye kauli mbiu ya 'Uzalendo ndio Ujanja'  Katikati ni Meneja Huduma za Utangazaji TCRA Mhandisi Andrew Kisaka na watatu kutoka kushoto Mwenyekiti wa TAMWA Joyce Shebe.
 

Meneja Huduma za Utangazaji TCRA,  Mhandisi Andrew Kisaka akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Dkt. Jabiri Bakari kuhusiana na Samia Kalamu Awards.
 

Sehemu ya wapiga picha katika utangazaji wa Samia Kalamu Awards
 

Baadhi ya waandishi katika utangazaji wa Samia Kalamu Awards

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...