Na Said Mwishehe,Michuzi TV

TANZANIA inatarajiwa kuwa Mwenyeji wa mkutano utakaohusisha wakuu wa nchi za Bara la Afrika kwa ajili ya kujadili masuala ya nishati sambamba na kuweka mikakati itakayofanikisha watu Milioni 300 katika bara hilo wawe wameungwanishwa na nishati ya umeme pamoja na nishati safi.

Sababu za Mkutano huo kufanyika Tanzania mwaka 2025 inatokana na Tanzania kuwa kinara na shamba darasa katika sekta ya nishati kutokana na hatua zinazochukuliwa na Serikali chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuweka mikakati ya kuendelea kuşambaza Umeme katika maeneo ya vijijini.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 16,2024 Jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dk.Dotto Boteko katika mkutano wa Tisa wa Soko la Nishati Barani Afrika ambao utafanyika nchini kwa siku mbili kuanzia leo na kesho na washiriki wanajadiliana kwa kina kuhusu nishati ya umeme.

“Kutokana na Tanzania kuwa Kama shamba darasa katika Enes la nishati katika Bara la Afrika , nchi yetu imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa mkutano wa nishati utakaohusisha wakuu wa nchi za bara letu la Afrika. Na hii inatokana na jitihada za Serikali chini ya uongozi wa Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kuweka mipango katika sekta ya nishati na mafanikio yetu ndio yanayofanya nchi nyingine za Afrika kuja kujifunza kwetu.

“Kupitia mkutano huo wa wakuu wa nchi utakaofanyika mwaka 2025 pamoja na masuala mbalimbali yanayohusu nishati kujadili pia watatoka na mkakati wa kufanikisha malengo ya kuhakikisha watu Milioni 300 katika Bara la Afrika wawe wanatumia nishati ya umeme ifikapo mwaka 2030.

“Jitihada ambazo Tanzania tunazifanya katika eneo la nishati hata Benki ya Maendeleo Afrika wamekuwa mashahidi kwani tumekuwa shamba darasa kwa nchi nyingine za Afrika lakini kwa uongozi wa Rais Dk.Samia na utekelezaji wa Ilani umeme umesambazwa kwa kiwango kikubwa katika vijiji vyetu.Hivyo mkutano huu wa leo utaweka maandalizi kuelekea mkutano wa wakuu wa nchini mwakani,”amesema Dk.Biteko.

Akieleza zaidi kuhusu Tanzania na hatua inazoendelea kuchukua katika sekta ya nishati Dk.Biteko amesema mbali ya kusambaza umeme vijijini Serikali pia inatambua kuwa nchi Jirani zinahitaji nishati ya umeme hivyo inaendelea na Ujenzi wa miundombinu kuhakikisha wanapeleka umeme katika nchi Jirani na kufafanua tayari wameshajenga miundombinu ya kupeleka umeme nchini Kenya na pale watakapohitaji umeme watapewa.

Pia amesema mbali ya Kenya pia imeundombinu ya umeme wa Tanzania inafanyika katika nchi za Rwanda ,Zambia pamoja na nchi nyingine jirani.Kwa upande wa nishati safi ya kupikia amesema jitihada mbalimbali zinaendelea na kwamba tayari Serikali imetoa ruzuku na mitungi 400,000 inaendelea kugawiwa kwa wananchi sambamba na wadau wengine kuungana na Serikali kutanikisha mpango wa nishati safi ya kupikia.

Hata hivyo amesema pamoja na kugawa mitungi hiyo wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi ili watumie mitungi ya gesi kwa usalama huku akisisitiza usalama wa mitungi ya gesi ni Mkubwa na ndio maana hakuna changamoto za matukio ya ya kulipuka kwa gesi ya majumbani.

Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika Dk.Kelvin Kairuki amesema kuwa mkutano huo unaondelea nchini Tanzania unalenga kujadili masuala ya nishati huku akisisitiza katika nishati Tanzania imepiga hatua na mkutano wa wakuu wa nchi unalenga kuendelea kuipigia debe Tanzania kwa jitihada inazofanya lakini pia kuipigia debe Afrika.

“Tumekubaliana na tutafanya kazi na Tanzania kwasababu katika nishati wako mbele, ndio maana hata kongamano la nishati mwakani litafanyika Tanzania na sababu ni kuipigia debe Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele katika nishati pamoja na Afrika kwa ujumla.”









Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...