Katika kusheherekea siku ya bia duniani, Kampuni ya Bia ya Tanzania (TBL), inayoongoza kwa utengenezaji wa vinywaji hapa nchini, leo imezindua Kampeni yake ya ‘Smart Drinking’ yenye lengo la kutoa elimu ya kunywa kistaarabu. Kampeni hii inalenga wauzaji na watumiaji wa bia ili kuwahimiza kunywa kwa kiasi na kwa usalama, na imefanyika katika kumbi mbalimbali za starehe katika mikoa ya Dar es Salaam, Mbeya, na Arusha.

Lengo kuu la Kampeni hii ni kuhakikisha watumiaji wa bia za Kampuni hiyo na wauzaji wanazingatia usalama wa afya zao kwa kunywa pombe kwa kiasi. Kwa kuwa wauzaji ni mabalozi wa kwanza wa bia hizi, wana jukumu kubwa la kuhakikisha wateja wao wanakunywa kwa njia salama na kistaarabu.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Bi. Michelle Kilpin, alielezea dhamira ya TBL katika kuwahamasisha wateja wake kunywa kistaarabu. "Kupitia kampeni hii ya ‘Smart Drinking’, tunawahimiza wateja wetu kutokuendesha vyombo vya moto wakiwa wametumia kilevi. Tunashauri pia watumiaji wapate chakula kabla ya kunywa bia na unywaji wa maji kila wanapokunywa bia," alisema Bi. Kilpin.

Aliongeza kuwa, "Lengo letu ni kupunguza ajali za barabarani zinazotokana na unywaji wa pombe kupindukia na kuzuia maradhi yanayosababishwa na matumizi makubwa ya pombe. Wauzaji wa bidhaa zetu wanapaswa kuwa waangalifu na kuacha kumhudumia mteja anayekunywa kupitiliza, na kumshauri arudi nyumbani."

Naye Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa TBL, Catherine Mabula, alifafanua kuwa kampeni hiyo imepata ushirikiano na mashirika mbalimbali ikiwemo Tanzania Red Cross Society (TRCS) maarufu kama Shirika la Msalaba Mwekundu, vilevile Polisi Tanzania pamoja na wauzaji wa bidhaa za TBL ili kuhakikisha jamii inakuwa salama. Aliongeza, "Kupitia Kampeni hii tunatarajia kwamba ajali za barabarani zinazotokana na unywaji wa pombe kupitiliza zitapungua kwa asilimia 10 kufikia 2025. Vilevile, tunaamini kuwa elimu hii itakua chachu ya kuboresha usalama wa wateja wetu.













Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...