Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Kassim amewataka vijana wa Kitanzania kutumia fursa za maendeleo ya kidigitali kama njia ya kujitengenezea fursa za ajira na kuacha kutumia mitandao ya kijamii kwa mambo yasiyofaa.
Mhe. Majaliwa amewataka vijana kufichua na kuziainisha taasisi zenye nia ovu ya kuharibu na kuvunja mila na desturi za Kitanzania, pamoja na taasisi hizo binafsi kujitambulisha na kutoa malengo ya Taasisi.
Katika kuadhimisha siku ya Vijana Kitaifa, Shirika lisilo la kiserikali la BRAC Maendeleo Tanzania,limeadhimia kuendelea na kuwekeza kwenye kutoa elimu zaidi kuhusiana na maendeleo ya vijana
Akizungumzia maadhimisho hayo, Meneja wa Mkoa Mwanza Novatus Tarimo amesema elimu wanayotoa kwa vijanai ni kuwawezesha vijana kupaza sauti kwa Serikali na jamii ili waweze kujiinua kiuchumi kupitia fursa mbalimbali zilizopo.
Amesema, Shirika la BRAC Maendeleo Tanzania limekuwa na miradi ya uwezeshaji kiuchumi kwa vijana na ikiwa ni katika kuunga mkono Serikali ya awamu ya sita kwa kuwainua kiuchumi na kuwapa fursa za kujiajiri.
Tarimo amesema, wao ni Wadau namba moja wa maendeleo na wamekuwa wakifanya kazi na Serikali kwa ngazi ya kitaifa na kuwekeza kwenye kutoa hamasa kutokana na matakwa muhimu kwa wakati huo.
"Vijana ndio taifa la kesho, kuna kila sababu ya kuwasaidia vijana hawa kwa kupaza sauti zao na kuwapatia elimu ya zaidi ili waweza kujiendeleza na kujiinua kiuchumi na kujiajiri,"amesema Tarimo.
"Mradi wa AIM, unaojihusisha na utoaji wa elimu na uwezeshaji wa kiuchumi na katika kipindi chote umekuwa na mafanikio makubwa sana,"
BRAC Maendeleo ni shirika lililojikita katika kuwezesha kiuchumi vijana kwa elimu ya ujasiriamali, na kwa kutoa mikopo ya vikundi kwa wakina.mama kupitia BRAC Finance Limited.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Kassim aizungumza na Vijana waliojitokeza katika viwanja hivyo amewataka vijana wa Kitanzania kutumia fursa za maendeleo ya kidigitali kama njia ya kujitengenezea fursa za ajira na kuacha kutumia mitandao ya kijamii kwa mambo yasiyofaa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Kassim aizungumza na Vijana waliojitokeza katika viwanja hivyo amewataka vijana wa Kitanzania kutumia fursa za maendeleo ya kidigitali kama njia ya kujitengenezea fursa za ajira na kuacha kutumia mitandao ya kijamii kwa mambo yasiyofaa.
Maandamano ya wafanyakazi na vijana wa BRAC Maendeleo Tanzania wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yaliyofanyika Jijini Mwanza.
Wananchi wakipita na kupata maelezo kutoka wafanyakazi wa BRAC Maendeleo Tanzania kuhusiana na uwezeshaji wa Vijana nchini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...