SHIRIKA la Wakala wa Huduma za Meli Nchini (TASAC) limewataka watanzania kuacha tabia ya kusafiri kwa kutumia vyombo vya majini vilivyopewa leseni ya kusafirisha mizigo kwani usalama wao upo hatarini.
Mkurugenzi Mkuu wa Tasac, Mohamed Salum ametoa tamko hilo jana wakati akizungumza na waandishi kwenye Maonyesho ya Saba ya Teknolojia ya Madini mjini Geita.

Alisema ipo kasumba ya baadhi ya wamiliki wa vyombo vya majini kwenda kinyume na leseni zao jambo ambalo hupelekea ajali za majini ambazo zingeweza kuepukika kwa kufuata utaratibu.

"Siyo unakuta mtumbwi wa uvuvi unapanda, au unakuta meli imebeba mizigo nawe unapanda, vyombo vya mizigo ni vya mizigo, na vina leseni ya mizigo," alisema.

Salum pia alikemea tabia ya baadhi ya watu kutumia mawakal amaboa siyo rasmi kuingiza mizigo nchini na kueleza kuwa Taasac inashirikiana na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) kukomesha tabia hiyo.

"Tasac tuna ushirikiano mkubwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania, kupitia kitengo chao cha forodha huwa tunapata taarifa kuna watu wanatumia mawakala ambao siyo Tasac kutoa huduma.

"TRA imekuwa ikiwakatalia na kuwapa maelekezo uingizaji wao lazima upitie Tasac kwa sababu za kiusalama ili serikali iweze kupata taarifa ya vitu vinavyoingia na kutoka," alisema.

Salum aliwataka wachimbaji wa madini wadogo, wa kati na wakubwa kuzingatia miongozo ya uingizaji wa vilipuzi na usafirirshaji wa makinikia hususani wa kupitia Tasac ili kungamua uhalali wa biashara yao.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...