· Benki ya Stanbic imekabidhi madawati 100 kwa shule ya sekondari ya wasichana Tulia na kwa shule ya sekondari ya Nsalaga.

· Sherehe ya makabidhiano ilifanyika katika shule ya sekodari ya wasichana Tulia na shule ya sekondari ya Nsalaga.

· Miche 200 ya miti, ikijumuisha ya kivuli na ya matunda imekabidhiwa kwa lengo la kuhamasisha uhifadhi wa mazingira

Stanbic Bank Tanzania inaendelea kuwekeza katika elimu na uhifadhi wa mazingira kwa kutoa madawati 100 na miche 200 ya miti kwa shule za mkoa wa Mbeya. Madawati hayo yatagawanywa kati ya Shule ya Sekondari ya Wasichana Tulia na Shule ya Sekondari ya Nsalaga, na sherehe ya makabidhiano imefanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Tulia.

Hatua hii inaonyesha dhamira ya Stanbic Bank ya kusaidia elimu na kuhamasisha uelewa wa uhifadhi wa mazingira nchini Tanzania. Mheshimiwa Beno Malisa, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini, aliongoza sherehe hizo, akiishukuru Stanbic kwa jitihada zake za kuinua jamii kupitia mipango ya Uwajibikaji wa Kijamii (CSR).

Mheshimiwa Malisa alitoa shukrani zake akisema, “Sisi kama serikali tunatambua mchango mkubwa wa Stanbic Bank kama mshirika muhimu katika kuunga mkono elimu. Pamoja na kutoa rasilimali muhimu kama madawati na miche ya miti, tunatambua pia uhitaji wa vifaa vya kidijitali kama vile kompyuta. Vifaa hivi ni muhimu katika kuwawezesha walimu na wanafunzi kuunganishwa na dunia na kuendana na maendeleo ya teknolojia, hivyo kuwaandaa kwa mazingira ya kisasa na ushindani.”

Akizungumza katika tukio hilo, Paul Mwambashi, Meneja wa Tawi la Stanbic Bank Mbeya, alisisitiza kujitolea kwa benki hiyo katika maendeleo ya jamii. “Katika Stanbic Bank, tunaamini katika kusaidia jamii tunazozihudumia, na tunajivunia kutoa rasilimali zinazochangia mazingira bora ya kujifunza na ya kijani kibichi,” alisema. “Msaada huu ni sehemu ya dhamira yetu ya kuleta athari chanya na yenye kugusa maisha.”

Msaada huo unajumuisha mchanganyiko wa miche ya matunda na miti ya kivuli, ikilenga kuunda utamaduni wa kuhifadhi mazingira miongoni mwa wanafunzi na jamii nzima. Kupitia mipango kama hii, Stanbic Bank inajitahidi kukuza maendeleo endelevu na kuchangia ustawi wa vizazi vijavyo vya Tanzania.

Hadi sasa, uwekezaji wa Stanbic Bank katika miradi ya maendeleo ya jamii umefikia TZS milioni 312, ukiathiri zaidi ya watu 104,660 nchini Tanzania. Madawati yanayotolewa yamezalishwa ndani ya mkoa wa Mbeya, ikionesha dhamira ya benki ya kusaidia biashara za ndani na kukuza uchumi wa ndani wa jamii. Kupitia mipango hii, Stanbic Bank haiungi mkono tu elimu, bali pia inachangia ustawi wa biashara za ndani.

Shughuli za CSI za benki hiyo zinajikita katika maeneo muhimu kama elimu, afya, uhifadhi wa mazingira, na maendeleo ya jamii. Stanbic Bank inabaki na dhamira ya kufanya michango yenye athari kubwa kwa ajili ya kuinua jamii na kukuza maendeleo endelevu nchini Tanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Mheshimiwa Beno Malisa (aliyevaa skafu), akiungana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Tulia kupokea msaada wa madawati 100 kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Wateja Binafsi na Mauzo kwa Wateja, Emmanuel Mahodonga, (watatu kutoka kulia), na Meneja wa Tawi la Mbeya, Paul Mwambashi, (wa pili kutoka kulia), pamoja na wawakilishi wengine wa benki hiyo. Madawati hayo, yaliyolenga kuboresha miundombinu ya elimu, yamegawiwa kwa usawa kati ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Tulia na Shule ya Sekondari ya Nsalaga, ambapo kila shule imepokea madawati 50. Juhudi hii inaonesha dhamira ya Benki ya Stanbic katika kuunga mkono elimu na kuiwezesha jamii katika Mkoa wa Mbeya. Hafla ya makabidhiano ilifanyika Jumatano mkoani Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mheshimiwa Beno Malisa (mwenye skafu)pamoja na wanajamii, wakipanda mti kama sehemu ya hafla ya kukabidhi madawati iliyofanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Tulia mkoani Mbeya. Zoezi la upandaji miti lilifuatia baada kukabidhi madawati 100 na miche 200 ya miti kutoka Benki ya Stanbic Tanzania kama sehemu ya Uwekezaji wake wa Kijamii. 

Madawati na miche ya miti viligawanywa kwa usawa kati ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Tulia na Shule ya Sekondari ya Nsalaga. Juhudi hii inahamasisha uhifadhi wa mazingira endelevu, ikisisitiza kujitolea kwa pamoja kuunda mustakabali wa kijani na kuongeza uelewa kuhusu kulinda rasilimali za asili kwa manufaa ya vizazi vijavyo. Tukio hili lilifanyika Jumatano mkoani Mbeya, likishuhudiwa na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kibenki kwa Wateja Binafsi na Mauzo Kwa Wateja Emmanuel Mahodonga, Meneja wa tawi la Mbeya Paul Mwambashi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...