Mtambo mkubwa wa kisasa aina ya Drilling Mashine ambao pia mbali na shughuli zingine pia ndio unaohusika kuchimba mashimo hayo katika eneo la mradi wa daraja hilo.
Mtambo mkubwa wa kisasa aina ya Drilling Mashine ambao pia mbali na shughuli zingine pia ndio unaohusika kuchimba mashimo hayo katika eneo la mradi wa daraja hilo.
Na Mwandishi Wetu,Pwani
DARAJA la Muhoro ambalo hivi sasa linasukwa kwa ustadi mkubwa na wa hali ya juu limesemekana kwamba baada ya kukamilika litatoa fursa kwa watanzania kufanya shughuli zao kwa ufanisi mkubwa.
Mbali na hilo pia watanzania wataweza kusafirisha bidhaa zao ikiwemo mazao pamoja na bidhaa zingine kwa ajili ya kujiingizia kipato kupitia kwenye daraja hilo.
Kubwa zaidi imeelezwa kuwa daraja hilo litaweza kuingiza watalii kwa wingi kutokana na kwamba watakuwa wanauwezo wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa urais zaidi tofauti na mwanzo ikizingatiwa eneo la Mbwela lina bichi mzuri sana kwani ni pembezoni mwa bahari ya Hindi ambapo maeneo hayo hayatumiki kwa sasa kutokana na kutokuwepo barabara na daraja hilo na baada ya hapa sasa yataanza kutumika.
Meneja Mkuu wa TARURA Pwani Rufiji Leopold Runji amesema kuwa mara baada ya kukamilika kwa daraja hilo mazao mbalimbali kama samaki, maembe, matikiti, nanasi, mastaferi,mpunga, mapapai, machungwa, mafenesi, maparachichi, nazi, korosho, na bidhaa zingine zitapitishwa kwenye daraja hilo na wafanyabiashara wa kitanzania kwa ajili ya kwenda kuuza na kujiingizi kipato.
Pia magari, bodaboda, watembea kwa miguu, baiskeri, maguta, magari makubwa vyote vitatumia daraja hilo kwa ajili ya kuingiza kipato kwenye Wilaya husika kwani pia kulikuwa mitambo ambayo ilishindwa kupita kwa ajili ya shughuli za kilimo, miradi ya ujenzi kwa ajili ya shughuli za kilimo, ujenzi wa barabara kwa kutumia madaraja vilikuwa vikisafilishwa kwa kutumia meri au boti.
Lunji anasema kuwa ujenzi wa daraja unaendelea vizuri katika hatua mbalimbali ambapo ujenzi wa maboksi karavati yamefikia asilimia hamsini na mawili yanaendelea kwenye ukarabati wakati ujenzi wa daraja kuu unaendelea kwa asilimia kubwa na kwamba mitambo inatengenezwa na kusukwa kwa asilimia sitini na kwamba mpango kazi ni kukamilisha kwa ndani ya muda wa wa mkataba.
Mhandisi Mkazi Emmanuel Mahimbo kutoka TREECO-Pwani katika Daraja la Mohoro, anasemwa daraja hilo linaendelea vizuri kutokana na kwamba watendaji wanafanya vizuri na wanajituma katika kuhakikisha kazi inatimia kwa wakati.
” Nipende kusema kuwa tuko vizuri katika utekelezaji wa jambo hili ambalo ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, kwani naamini baada ya hapa hakuna mwananchi atakayeweza kulalamika,” alisema Mahimbo na kuongeza kuwa,
“Lakini nipende kuweka wazi kuwa Teknojia inayotumika haina kiswahili badala yake inaitwa [CFA] Continuase Flaith Auge, ambapo vyovyote itakavyokuwa mvua ikinyesha hakuna cha kuendelea ila kinachotakiwa ni kumaliza kabla ya mvua hazijanyesha.
Aidha, alisema kutokana na mpango huo wa Mhandisi Mshauri na Mkadarasi ambao wamejipanga vizuri matarajio yake ni kwamba kabla ya mvua hizo kuendelea chini ya daraja patakuwa pamekamilika kumaliza na kukamilika kwa wakati.
Hata hivyo hakusita kama Taasisi wanayomatario makubwa ya kuongeza pato la Serikali kupitia kwa mama yetu Rais wa Nchi Samia Suhuhu Hassan kutokana na jinsi alivyowezesha miradi hii na sasa tunaamini wananchi wetu wanamatumaini ya kuwa na maendeleo makubwa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...