Na Mwandishi Wetu
Viongozi wametakiwa kutekeleza majukumu ya kusimamia utoaji wa elimu ya mikopo kwa wananchi na kuhakikisha wanapata mikopo kwa kuzingatia haki .
Hayo yamezungumzwa Novemba 25,2024 na mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo wakati wa mafunzo kwa viongozi juu ya urejeshwaji wa mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na wenye ulemavu, yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Anatoglo jijini Dar es salaam.
Mpogolo amesema kuwa viongozi wanatakiwa kuzingatia walengwa katika utoaji wa mikopo kwa kuangalia wale walioanzisha vikundi ambavyo vipo ili kuleta mabadiliko katika wilaya ya Ilala.
Aidha amewataka viongozi hao kupokea mapendekezo yaliyoletwa ili kutoa mikopo kwa vikundi vya wanawake,vijana na wenye ulemavu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa jiji la Dar es salaam Ndugu Elihuruma Mabelya amesema viongozi wanatakiwa kutoa elimu ya mikopo na hamasa kwa wananchi ili wapate kujitokeza katika kuchukua mikopo hiyo.
Pia ametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha wananchi wanawezeshwa kiuchumi ili waweze kufikia malengo yao.
Pamoja na hayo katika mafunzo hayo viongozi mbalimbali waliapishwa kulingana na vyeo vyao kwa makundi matatu ikiwemo kundi la menejimenti,kamati ya huduma ya mikopo na kamati ya uhakiki kwa ngazi ya wilaya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...