Na Lilian Ekonga. Dar es salaam.

Tanzania  kupitia  shirika la uwakala  wa Meli Tanzania (TASAC) imeteuliwa  kuwa  nchi mwenyeji kwenye  wa Makutano wa  saba (7) wa akimataifa wa jumuiya ya  Mamlaka za usimamizi wa usafiri  Majini Barani Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe  29 novemba  hadi 10 Disemba 2024 jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Waziri  wa Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amesema lengo la mkutano  huo ni kujadili  masuala muhimu  ya maendeleao ya udhibiti na usimamizi wa usalama wa usafiri majini hatani afrika.

Amesema  kipaumbele kikiwa ni mustakabali wa usafiri wa majini ma kuongeza ushirikiano baina ya nchi na wanachama.

"Kauli mbiu ya mkutano huo ni ' Kuimarisha mustakabali wa sekta ya usafiri majini barani Afrika, ushirikianao katika teknolojia na ubunifu  ili kupunguza hewa ukaa, kuimarisha  usalama wa mazingira,  na  mazingira  ya sekta ya usafiri majini  kwa mustakabali endelevy"amesema

Ameongeza kuwa  mkutano utafunguliwa  na  Naibu Waziri Mkuu  na Waziri wa Nishati Dkt Dotto Biteko na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa shirika la Bahari Duniani, Bw Antonio Dominguez pamoja na wataalam wa usafiri majini, viongozi wa mamlaka za udhibiti wa usafiri kutoka nchi na wanachama  wa umoja wa Afrika  zipatazo 50 ambazo zina bahari.

Pia Waziri  amesema  mkutano huo  utatatumika kama jukwaa muhimu katika kuwezesha wadau kushiriki katika  majadiliano yanayogusa masuala ya teknolojia na ubunifu yenye kulenga katika kuimarisha usalama wa usafiri majini.

"Ushiriki wa Bw. Dominguez ni heshima kubwa kwa Tanzania  hasa kipindi  hiki tunapotekeleza sera  ya Taifa ya uchumi wa Buluu ambapo  kama nchi tumebainisha  masuala ambayo serikali  kwa kushirikiana na Wadau" amesema waziri Biteko

Aidha amebainisha Tanzania  itaendelea kutangaza  fursa za kiuchumi zilizopi katika sekta  ya usafiri  kwa  njia ya maji zinazohusiana  na utumiaji  wa rasilimali za habari na maziwa zitakazo saidia  kuongeza uwezo wa  serikali kuwa hudumia  wananchin na kuwaletea maendeleo.

Alikalika ametoa wito  kwa wadau wa sekta  ya usafiri majini, wakiwemo wasafirishaji, wamiliki wa vyombo vya  usafirishaji majini, wawakilishi wa  mashirika ya kimataifa, viongozi  wa serikali kujitokeza  kwa wingi kuhudhuria mkutano huo muhimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...