NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

UFUNDISHAJI wa elimu ya Katiba na Uraia katika shule za msingi, sekondari na vyuo vya mafunzo ya Ufundi Stadi itawezesha kizazi kijacho kuwa chenye maadili, ujuzi, maarifa, wazalendo wa kweli na wenye kuipenda nchi yao.

Hili ni jambo jema na la kuungwa mkono, kwani Taifa linahitaji kizazi chenye uzalendo ili kuenzi na kudumisha amani ya Nchi.

Hayo yameelezwa leo Novemba 28,2024 Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na SheriaDkt. Franklin Rwezimula wakati akifungua kikao cha kupitishwa kwenye mpango kazi wa ufundishaji wa elimu ya katiba na uraia katika shule za msingi, sekondari na vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi.

Amesema elimu hiyo ni muhimu kwa kizazi cha sasa kwani kuna changamoto kadhaa katika nchi yetu hususani suala la uelewa mdogo wa uzalendo na maadili pamoja na misingi ya haki za binadamu, mambo ambayo husababisha taharuki katika jamii zetu.

"Suala hili likikamilika na elimu ya Katiba na Uraia ikianza kutolewa, itakuwa chachu ya kuleta mabadiliko chanya miongoni mwa jamii yetu, kuongeza uzalendo katika mioyo na akili za wanafunzi wetu, utii kwa Katiba ya Tanzania, kuimarisha umoja wa kitaifa, kukuza ushiriki wa Kidemokrasia na kudumisha amani na utulivu nchini". Amesema

Aidha, amesema kuwa elimu ya Katiba na Uraia itasaidia kuandaa vijana wanaozingatia haki na wajibu wao kwa nchi yao ya Tanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Anthony Kasore amesema ufundishaji wa somo hilo VETA, itasaidia vijana wanaomaliza masomo yao kuwa na uzalendo na kwenda kuitetea nchi yao kimaendeleo.

"Kijana tukimpitisha kwenye mafunzo haya, akafahamu ni nini anatakiwa kufanya kama kijana wa kitanzania na baadae kuona umuhimu wa kulipa kodi kwaajili ya kusaidia maendeleo ya nchi yetu kwa ujumla". Amesema Kasore


















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...