Na Mwandishi Wetu, Michuzi Tv

KAMPUNI ya Dhahabu ya Barrick (NYSE:GOLD)(TSX:ABX) imepokea kwa furaha uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Ontario wa kutupilia mbali madai yaliyotolewa na wakazi wa Tanzania waliokuwa wakilalamikia ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania jirani na mgodi wa dhahabu wa kampuni hiyo wa North Mara.

Mahakama hiyo imeamua kwamba Ontario haikuwa jukwaa mwafaka la kusikiliza madai hayo.

Rais na Mtendaji Mkuu wa Barrick, Mark Bristow, amesema kampuni hiyo imekanusha mara kwa mara kile inachokiona kama madai yasiyo na msingi yanayotolewa asasi chache zisizo za serikali zenye mrengo wa kianaharakati zinaodai kuwapo kwa ukiukwaji wa kihistoria wa haki za binadamu katika maeneo yanayozunguka mgodi wake wa North Mara.

“Tunajivunia mafanikio tuliyoyapata nchini Tanzania kutokana na ushirikiano wetu na Serikali ya nchi hiyo kupitia ubia wa Twiga. Mchango wa mapato ya migodi yetu umeleta mageuzi katika uchumi wa nchi hiyo wakati uwekezaji wetu katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya jamii za wenyeji, ukiambatana na mkakati wetu wa kuleta maendelea ya jumla, umeboresha hali ya maisha yao," amesema.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...