Na Mwandishi wetu - Dar es salaam


Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Zuhura Yunus, amewahimiza Madereva kuzingatia tija na ufanisi katika utendaji kazi  ili kuhakikisha jamii inafanya kazi  za kiuchumi kwa usalama, kukuza uchumi  wao na uchumi wa  Taifa kwa ujumla

Ameyasema hayo leo Novemba 28, 2024 wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya ustadi wa kuboresha Tija na Ufanisi kwa madereva jijini Dar es Salaam. 

"Changamoto ya ajali barabarani zinaathiri nguvu kazi ya Taifa na kupunguza pato, hivyo basi ni muhimu kuzingatia mafunzo haya ili kupunguza ajali ambazo zinaweza kuepukika" amesema

Awali akizungumza Mkurugenzi wa Ukuzaji Tija, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Yohana Madadi, amesema lengo la Mafunzo hayo ni kutoa ujuzi na mbinu za udereva bora ili kupunguza ajali barabarani na kutii sheria bila shuruti.






 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...