Balozi wa mbio  hizo Twaha Ambiere  akizungumza kwenye uzinduzi  huo.


Na Khadija Kalili Michuzi Tv
IKIWA imezoeleka kuwa kwenye mbio kunakua na vituo vya kutoa maji ya kunywa kwa wakimbiaji imekua tofauti kwa waratibu wa Coast City Marathon wamesema kuwa wao watatoa maji ya dafu na supu ya pweza.

Katika maboresho ya mbio za mwaka huu Coast City Marathon tumeamua kunogesha kwa kuwa na vituo vitakavyokua vinatoa maji ya madafu na supu ya pweza kwa wakimbiaji ikiwa ni katika kuenzi utamaduni wa Mkoa wa Pwani.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo ya taehe 11, Novemba 2024 kwenye uzinduzi rasmi wa mbio hizo Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo Dkt. Frank Mhamba amesema kuwa mbio hizo zitafanyika Novemba 30 mwaka huu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kibaha Theresia Everist Kyara amesema kuwa wote tunafahamu kuwa serikali yetu inatumia fedha nyingi katika kupambana na magonjwa yasiyo ambukiza hivyo natoa wito kwa wananchi wote wa Kibaha na amaeneo jirani na Mkoa wa Pwani kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye mbio hizi na kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi.

Kyara amesema kuwa kiasi cha fedha zitakazopatikana zitakwenda kuboresha miundombinu ya Shule ya Msingi Pangani kwa kujenga jengo la Utawala ambapo shule hiyo ipo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani.

Naye mwakilishi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi Judith Mwinuka amesema kuwa wanatoa ahadi ya kushiriki kwa wingi sambamba na kutoka huduma za afya kwa washiriki kama ilivyokua kwenye msimu uliopita.

Balozi wa mbio hizo hizo Twaha Ambiere amesema kuwa kutakua na mbio za watoto 2.5Km 5Km,10Km,15 Km na 21Km pia amesisitiza usajili ni kiasi cha 35, 000 kwa kila mmoja ambapo mshiriki atapata medali ,fulana pamoja na riboni ya mkononi.

Amesema kwa mbio hizo za Coast City Marathon zinafanyika kwa mara ya tatu sasa huku zikiwa zinachagiza kukuza sekta ya michezo na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali kwenye jamii.

Ambiere, ametoa hamasa kwa wadau kujitokeza kwa wingi kujisajili ili waweze kushiriki kikamilifu.

Mbio hizo zimedhaminiwa na CRDB, NSSF, TIGO,DAVIS&SSHIRTLIFE na wengine wengi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...