Ili kufanikisha azma ya kujenga haki na usawa kiuchumi kwa wanawake nchini, Serikali ya Tanzania na taasisi za maendeleo katika jamii wanatekeleza afua mbalimbali za kiuchumi katika jamii kwa lengo la kujenga mazingira bora ya ufanyaji wa kazi za kiuchumi.


Moja wapo ya afua hizi ni kuanzishwa kwa majukwa ya uwezeshaji kiuchumi kwa wanawake nchi nzima.


Historia ya majukwaa ya uwezeshaji kiuchumi wanawake inaanzia mwaka 2016 ambapo aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alimteua, wakati huo Makamu wa Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika jopo la Umoja wa Mataifa la kuangalia namna ya kuongeza ushiriki wa wanawake katika uchumi duniani.


Baada ya uteuzi wake katika jopo hilo la kimataifa, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan wadau wa uchumi hapa nchini waliunda Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi Wanawake Tanzania.


Mheshimiwa Samia alilizindua Juni 2016 na kuagiza majukwaa hayo kuundwa kila mkoa, jukumu ambalo lilikabidhwa kwa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na iliyokuwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Wanawake.


Kwa mujibu wa mwongozo wa uanzishwaji na uendeshaji wa Majukwa ya Uwezeshaji Kiuchumi Wanawake, malengo ya Jukwaa ni kuwakutanisha wanawake ili wajadili fursa mbalimbali za kiuchumi na changamoto wanazokutana nazo wakati wa utekelezaji wa shughuli za kiuchumi nchini.


Mkoani Lindi ambako majukuwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi yameundwa tangu mwaka jana tu, kuna kila sababu ya kuwa na matumaini kuwa majukwaa haya yanaleta na yataleta matokeo chanya na kukidhi makusudi ya uanzishwaji wake.


Kamati ya ushauri ya kitaifa kuhusu kizazi chenye usawa, inaendelea kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa kazi za majukuwaa ya uwezeshaji kiuchumi wanawake kwa kuwa ni nyenzo muhimu ya upatikanaji wa haki na usawa kiuchumi.


Kamati hii ya wajumbe 26 inayoongozwa na Mheshimiwa Angela Kairuki, mshauri wa rais, na Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mheshimiwa Mgeni Hassan Juma, imekuwa ikifanya ziara sehemu mbalimbali za nchi kujionea mafanikio na changamoto za majukwaa haya na kutoa ushauri kwa lengo la kuhakikisha malengo ya majukuwaa haya yanafikiwa.


Kufikia mwaka 2023, mkoa wa Lindi ulikuwa na majukwaa ya uwezeshaji kiuchumi tangu ngazi ya kijiji, kata, wilaya na mkoa, kwa mujibu wa Angel Julius Kessi, Mwenyekti wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi Wanawake Mkoa wa Lindi.


Faida mojawapo ya majukwaa haya ya uwezeshaji ni kuwakutanisha wanawake wenye nia ya kujiendeleza kiuchumi na wadau ambao wana nia ya kuwawezesha.


Aghalabu wadau wa maendeleo hupendelea kuwekeza kwa watu ambao wameonesha nia kwa vitendo kwa kuanzisha shughuli ya kiuchumi, kujiunga pamoja katika vikundi vya kimaendeleo ama kuanza kufanya biashara ama uzalishaji flani.
Wanachama wa jukwaa wamekuwa wakipata semina mbalimbali toka wa taasisi za fedha, serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali. Taasisi za kifedha zilizoko mkoa wa Lindi zimekuwa zinatoa umuhimu sana kwa wanachama wa jukwaa la uwezehshaji.


“Kweli tumeona wadau mbalimbali wamekuja kuonana na wanawake wajasiriamali katika sekta mbalimbali na wengi wamepata fursa zao mafunzo ya kuboresha kazi zao, wemepata taarifa za masoko na mengine mengi,” anasema Kessi.


Kando na wadau wanaokuja jukwaa la uwezeshaji wanawake kiuchumi limekua likiandaa makongamano tofauti kuwaleta wanawake wanaofanya kazi mbalimbali za kiuchumi
fursa inayofanya vizuri katika vikundi vya wanawake wa mkoa wa Lindi ni kilimo cha mwani, ambao hulimwa Kitumbi kwera, Kilwa na Mchinga.


Pamoja na kwamba wengi wa wakulima wa mwani walikuwa na vikundi vyao kabla ya uanzishwaji wa jukwaa la uwezeshaji kiuchumi, ujio wa jukwaa umeongeza tija ya umoja kwa kuwatambua wakulima kwa wingi wao ambao ni raslimali kibiashara.


Kupitia jukwaa la uwezeshaji kiuchumi, wakulima wa mwani wamepata mafunzo ambayo yamewapa ujasiri kuendelea kulima mwani kama zao la kuu la biashara, hata kama bei ya mwani ghafi imekua ikiendelea kushuka.


Sokoni bei za mwani ambayo ilikuwa Tshs 5000/- kwa kilo mwaka.. ilishuka hadi 2,500/-, 2,000/- na hatimaye mwaka huu, wakulima wanaouza mwani ghafi wanalizimika kuuza kwa Tshs 1,500/-.


Wakulima wa mwani wa vikundi ambavyo vimeshapata mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa zinazotokana mwani hawana wasiwasi na kuporomoka kwa bei ya mwani ghafi. Bidhaa za mwani zinalipa kuliko kuuza mwani ghafi, zinadumu na zinaweza kusafirishwa mbali zaidi bila kuharibika.


Mwani uliosagwa unaweza kuuzwa kwa Tshs 15000/- au zaidi. Kipande cha sabuni ya malighafi ya mwani kinauzwa Tshs 2000/- na mafuta ya mwani chupa ya mililita 150/- inauzwa hadi Tsh 5,000/-


“Mafunzo tuliyopata ya kutengeneza bidhaa za mwani yamenifanya nijiamini zaidi kuhusu ukulima wangu wa mwani,” anasema Mwishura Ali from Tuwenao group. Mwashira alianza kulimwa mwani kitambo, alishakatishwa tamaa na kuporomoka kwa bei.


“Tuliona haya mabadiliko baada ya wataalamu toka wilayani kuja kutupatia mafunzo, Sina wasiwasi tena kwa kuwa hata kama bei ya ghafi ikishuka bidhaa za mwani nazotengeneza zinadumu na nitaendelea kuziuza kwa faida,” anasema.


Mkulima mwingine, Mwajuma Mohamed Majonde, kutoka wilaya ya Mchinga in Lindi alianza ulimaji wa mwani akiwa kikundi inachoitwa Umoja. Ndani ya kikundi, alijifunza kilimo na uandaani wa bidhaa za mwani kupitia mafunzo mbalimbali.

“Nimeamua kuendelea na kikundi na kuwa na biashara yangu ya uandaaji wa bidhaa. Ninatengeneza shampoo, sabuni, mafuta ya kujipaka na lotions. Pia ninawafundisha wanawake na yeyote anayehitaji kujifunza kuhusu utengenezaji wa bidhaa,” anasema.

Kupitia kuunganishwa na vikundi kupita jukwaa ameshawapatia mafunzo wanawake kwenye vikundi zaidi ya kumi.

Majukwaa pia yanawapa wanawake fursa ya changamoto zao kuonekana haraka na ufumbuzi kuanza kutafutwa. Kwa wakulima wa mwani wa Lindi, changamoto ambayo inafanyiwa kazi kwa sasa ni kutafuta makaushio ya kisasa. Kawaida wakulima wa mwani kuhausha chini kwenye mchanga. Hii inapunguza thamani ya mwani na wakulima hupata hasara wakati wa mvua wakati jua halitoshi kukausha.

“Tumefanya mazungumzo ya awali na wadau mbalimbali ili kuwapatia wakulima wa mwani teknolojia ya kukausha mwani kwa kutumia umeme jua. Hii itawezesha wakulima wa mwani kukausha mwani wao mwaka wote bila kuwepo usumbufu,” anasema Kessi.

Ni vyepesi kuanzisha mazungumzo na kampuni zenye teknolojia sadifu kwa kuwa ukubwa wa tatizo unajulikana kwa kuwa wakulima wanaunganishwa kupitia, vikundi vyao ambavyo vinajulikana ndani ya jukwa uwezeshaji.

Kadri dunia inavyonjea kuelekea mwaka 2030 kukamilisha malengo ya maendeleo endelevu, Tanzania bila shaka chombo hiki cha uwezeshaji kiuchumi kitaendelea kutoa mchango mkubwa ili kuyafikia malengo ya kitaifa na kimataifa ya kujenga kizazi chenye usawa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...